FURSA ZA UWEKEZAJI WA UCHUMI NA VIWANDA WILAYANI RUNGWE
Utangulizi
Ili kuongeza soko kwa bidhaa zinazopatikana Wilayani, Halmashauri inaendelea na jitihada ya kutafuta maeneo yanayofaa kwa uwekezaji wa soko/kiwanda ambapo kwa kushirikiana na wadau lengo la uboreshaji wa huduma kwa kuanzisha viwanda litatimia. Maeneo yanayotafutwa ni kama yafuatayo;-
Maeneo yanayomilikiwa na Serikali kama Serikali ya Kijiji, Halmashauri n.k
Maeneo ambayo Serikali inaweza kuyamiliki kwa kununua au kulipa fidia.
Maeneo yanayomilikiwa na wananchi ambao wapo tayari maeneo yao yatumike kwa uwekezaji kwa makubaliano maalum.
Hadi kufikia Septemba 2017, Maeneo yaliyopatikana kwa ajili ya uwekezaji ni:-
NA
|
ENEO LILIPO (KIJIJI)
|
UMILIKI
|
UKUBWA WA ENEO
|
AINA YA MATUMIZI YANAYOPENDEKEZWA
|
1.
|
Kijiji cha Ilenge jirani na ATTI
|
Halmashauri
|
Ekari 10.67
|
Soko la ndizi
|
2.
|
Kijiji cha Ilenge eneo lililotolewa na TANROAD
|
Halmashauri
|
Ekari 2
|
Kiwanda cha kati cha kusaga kahawa na kokoa
|
3.
|
Kijiji cha Ilenge kituo cha Rasilimali ya wakulima
|
Halmashauri
|
Ekari 15
|
Kiwanda cha kati cha maziwa
|
4.
|
Kijiji cha Unyamwanga
|
Halmashauri
|
Halijapimwa
|
Kiwanda cha kati cha crips (Viazi)
|
5.
|
Kijiji cha Mbeye I
|
Binafsi
|
Ekari 3
|
Soko/ kiwanda cha viazi
|
6.
|
Kijiji cha Ilundo
|
Serikali ya Kijiji (Hati)
|
Ekari 38
|
Ufugaji wa samaki
|
7.
|
Kijiji cha Ilundo
|
Serikali ya Kijiji(Hati)
|
Ekari 9
|
Soko la ndizi
|
Aidha Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya imepata taarifa ya kuwepo maeneo yanayofaa kwa uwekezaji. Maeneo hayo ni:-
Kijiji cha Lupoto
Kijiji cha Lugombo
Kijiji cha Kikota
B) TAARIFA UTALII
YAFUATAYO NI MAENEO YALIYOAINISHWA KUFANIKISHA MIKAKATI YA KUENDELEZA NA KUTANGAZA SHUGHULI ZA UTALII
NA |
AINA/JINA LA KIVUTIO |
ENEO KILIPO(KATA) |
MIKAKATI/ MPANGO |
MUDA WA UTEKELEZAJI |
HALI YA UTEKELEZAJI |
MAELEZO/ MAONI |
1.
|
Hifadhi ya Mlima Rungwe
|
Isongole, Ndanto, Kiwira, Ikama, Suma
|
-Kuboresha miundombinu ya barabara, mabango,vyoo, mageti na kambi za kupumzikia Wageni
-Kutangaza eneo hili kwa kutumia vipeperushi,TV na mitandao ya kijamii |
2017/18 – 2018/19
|
-Choo kimoja kimejengwa, geti, nyumba ya kupokelea wageni, mabango, vimbweta na barabara ya Ngumbulu imeboreshwa
|
-Halmashauri inaendelea na uhamasiahaji Wadau kutumia fursa za Uwekezaji wa huduma za Watalii (hoteli,mabanda,migahawa na kwa kushirikiana na TCCIA na TIC.
|
2. |
Ziwa ngozi
|
Isongole, Swaya na Ndanto
|
Kuboresha miundombinu ya barabara, mabango,vyoo,mageti na kambi za kupumzikia wageni
-Kutangaza eneo hili kwa kutumia vipeperushi, TV mitandao ya kijamii na Mabango yanayoingia eneo la H/W |
2017/2018 |
-Vimbweta 6 vya kupumzikia wageni vimejengwa
-Eneo limetangazwa |
-Uhamasishaji unaendelea kutumia fursa za uwekezaji wa huduma za Watalii (hoteli, mabanda, migahawa). Andiko linaandaliwa na litawasilishwa kwa Wadau kuanzia mwezi Novemba, 2017 ili kusaidia juhudi za H/W.
|
3. |
Daraja la Mungu
|
Lupoto
|
Kuboresha miundombinu ya barabara, mabango, vyoo, mageti na kambi za kupumzikia wageni
-Kutangaza eneo hili kwa kutumia vipeperushi,TV na mitandao ya kijamii |
2017/2018 - 2018/2019 |
Choo kimoja kimejengwa
-Mabanda 3 ya kupumzikia wageni na mabango 2 yamewekwa |
Uhamasishaji unaendelea kutumia fursa za uwekezaji wa huduma za Watalii (hoteli, mabanda, migahawa).
|
4. |
Maporomoko ya Maji Kapologwe
|
Kisondela
|
Kuboresha miundombinu ya barabara, mabango,choo,uzio.
-Kutangaza eneo hili kwa kutumia vipeperushi,TV na mitandao ya kijamii. |
2018/2019 |
Barabara imeboreshwa na inafikika.
|
Halmashauri inaendelea na uhamasishaji Wadau kutumia fursa za uwekezaji wa huduma za Watalii (hoteli, mabanda, migahawa).
|
5. |
Ziwa Kisiba
|
Kisiba
|
Kuboresha miundombinu ya barabara, mabango,choo,uzio
-Kutangaza eneo hili kwa kutumia vipeperushi,TV na mitandao ya kijamii |
2017/2018-2018/2019
|
Barabara imeboreshwa na inafikika
|
Uhamasishaji unaendelea kutumia fursa za uwekezaji wa huduma za Watalii (hoteli, mabanda, migahawa. Tayari wadau wameanza kujitokezakuwekeza.
|
6. |
Maporomoko ya maji malasusa, Kapiki
|
Nkunga
|
Kuboresha miundombinu ya barabara, mabango,choo,uzio
|
2019/2019 |
Barabara imeboreshwa na inafikika, bango limewekwa
|
Wadau wanaendelea kuhamasishwa kutumia fursa za uwekezaji wa huduma za Watalii (hoteli, mabanda, migahawa.
|
7. |
Maji moto Ilwalilo
|
Kisiba
|
Kuboresha miundombinu ya barabara, mabango,choo,uzio na mabanda ya kupumzikia wageni
|
2019/2020 |
- |
Fursa za uwekezaji wa huduma za Watalii (hoteli, mabanda, migahawa zinaendelea kutangazwa kwa Wadau ili wawekeze.
|
8 |
Maporomoko ya Isabula, Ngomano,
|
Kisiba,
Lupepo |
Kuboresha miundombinu ya barabara, mabango,choo,uzio
|
2020/2021 |
- |
Uhamasishaji Wadau kutumia fursa za uwekezaji wa huduma za Watalii (hoteli, mabanda, migahawa unaendelea.
|
9. |
Mti Katembo
|
Kisiba
|
-Kuboresha miundombinu ya barabara, mabango,choo,uzio
-Kutangaza eneo hili kwa kutumia vipeperushi,TV na mitandao ya kijamii |
2018/2019 |
- |
Halmashauri inaendelea na uhamasishaji Wadau juu ya fursa za uwekezaji wa huduma za Watalii (hoteli, mabanda,migahawa).
|
10. |
Misitu ya matambiko(Kasisi na Kabale)
|
Nkunga, Suma
|
Kuboresha miundombinu ya barabara na mabango.
|
2018/2019 |
- |
Halmashauri inaendelea kuhamasisha Jamii kutembelea maeneo ya Asili yaliyopo Wilayani.
|
11
|
Majengo ya kale
(Kambi za kale za Wajerumani) |
Kisiba, Bulyaga(Boma)
|
Kuboresha maeneo hayo kuwa maeneo ya kitamaduni na Kumbukumbu za mambo ya kale.
|
2019/2020 |
- |
Uhamasishaji unaendelea kwa Jamii kutembelea Mali Kale zilizopo Wilayani.
|
12
|
Kambi ya Uvuvi Isongoe
|
Isongole
|
Eneo hili limetangazwa kwa ajili ya uwekezaji wa Kambi ya Utalii.
|
2017/2018 |
Eneo limepimwa na kufanyiwa uthamini
|
Halmashauri inaendelea kuzitambua na kuhamasisha Wadau kutumia fursa za uwekezaji wa huduma za Watalii zilizopo Wilayani.
|
NB: Ili kutangaza vema vivutio na kujenga uelewa wa jamii juu ya uwepo wa Vivutio vya Utalii vilivyopo Wilayani, Halmashauri ya Rungwe inaendelea na ukamilishaji utengenezaji mabango mawili yenye urefu wa mita 2 na upana wa mita 1.5 kila moja ambayo kwa pamoja yamegharimu Sh. 1,300,000/=. Mabango haya, yatawekwa maeneo ya mpakani na Wilaya za Mbeya Vijijini eneo la Kijiji cha Isyonje, Kata ya Isongole na mpakani na Wilaya ya Kyela eneo la Kijiji cha Ilima, Kata ya Ilima.
SEKTA YA BIASHARA
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa