• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Rungwe District Council
Rungwe District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa naSerikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango, Uchumi na Takwimu
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, U mwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Usafishaji na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Tehama na Mahusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Utunzaji Nyuki
  • Uwekezaji
    • Uzalishaji wa Maziwa
    • Kiwanda Cha Matunda
    • Vivutio vya Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Ardhi na Maliasili
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
      • Mikutano ya Madiwani
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu za Maombi
    • Katiba Pendekezwa
    • Mihutasari
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
    • Matukio
    • Habari
    • Makala

Mifugo na Uvuvi

 MUUNDO WA IDARA YA MIFUGO NA UVUVI NA SHUGHULI ZINAVYOTEKELEZWA KWA KILA SEKTA 

A.AFISA MIFUGO NA UVUVI

  1. Kutafsiri Sera,miongozo,sheria,kanuni zinazo husiana na mifugo na uvuvi
  2. Kuhamasisha utafiti unaohusiana na shughuli za mifugo na uvuvi ngazi ya wilaya hadi kijiji
  3. Kuhamasisha wadau mbalimbali kama asasi zisizo za kiserikali,makampuni ya biashara,benki na wadau wengineo kuwekeza katika sekta ya mifugo na uvuvi
  4. Kufuatilia mikataba, na zabuni za miradi ya mifugo kuhakikisha zinaingiwa kwa muda unaotakiwa pamoja na kusimamia mikataba
  5. Kushirikiana na Taasisi zingine za serikali ambazo ni mtambuka katika kutekeleza majukumu yake kama Afisa maliasili,Afisa mazingira,Afisa ardhi,Ofisi ya mkuu wa Mkoa vituo vya mafuzo ya mifugo na vituo vya uchunguzi wa maradhi ya mifugo
  6. Kuratibu shughuli zote zinazofanywa na serikali, taasisi mbalimbali za serikali na sekta binafsi na kutoa taarifa kama kunatatizo linalokinzana kisheria na kutoa utatuzi au mapendekezo ya utatuzi kwa tatizo linalojitokeza.
  7. Kuandaa taarifa za mifugo na uvuvi na kuwasilisha katika ngazi mbalimbali za Halmashauri,mkoa na taifa
  8. Kuandaa taarifa watumishi wa mifugo kwa mwaka
  9. Kusimamia ubora wa pembejeo za mifugo na uvuvi zinazoingia,tumika na kutoka wilayani
  10. Kutekeleza majukumu ya kiserikali yatakayotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri.

B-AFISA UGANI MSHAURI WILAYA

Kuwajengea uwezo maafisa mifugo wa kata na vijiji namna ya kuunda vikundi na kufanya kazi na vikundi vya wafugaji pamoja na kuhakikisha kuwa elimu inayotolewa kwa wafugaji ni sahihi (kupitia vipeperushi,mabango na vyombo vingine vya habari.)

Kuanzisha, kuendeleza na kusimamia mashamba darasa ya mifugo pamoja na kusimamia tafiti zinazoendeshwa katika mashamba darasa yaliyoko kwenye kata mbalimbali kwa kuzingatia sheria taratibu na kanuni za mifugo.

Kuanzisha na kuhamasisha elimu ya ufugaji wa mifugo katika Halmashauri kwa njia ya vipeperushi,vikundi na jukwaa la wafugaji pamoja na kuandaa mikutano ya wadau wa mifugo ngazi ya Halmashauri.

Kuibua na kuandaa bajeti ya mifugo ya mwaka kutegemeana na vipao mbele vilivyoiburiwa ngazi ya kata na vijiji na kutengeneza mpango kazi mahususi wa mwaka husika ngazi ya Halmashauri.

Kumsaidia afisa mifugo na Uvuvi kuandaa miongozo ya ugani katika wilaya na kuwezesha miongozo hiyo kufika ngazi ya kata na vijiji.

Kujenga mahusiano na kuhamasisha makampuni binafsi kuwekeza/kushiriki katika shughuli za ugani kwa sekta ya mifugo

Kuandaa na kuunganisha taarifa za robo na za mwaka za shughuri za ugani na kuziwakilisha kwa afisa mifugo na uvuvi wilaya kwa wakati.

Kufanya shughuli za kiutawala na kiutaalamu kama utakavyoagizwa na Afisa mifugo/Uvuvi wa wilaya.

C-DAKTARI WA MIFUGO 

Daktari wa mifugo anapaswa kutumia muda mwingi nje ya ofisi ili kuweza kubaini magonjwa mbalimbali katika machinjio,  mipakani ,hospitalini na kwenye mabanda ya mifugo ya aina zote ili kujua viashiria vya magonjwa na hivyo kuwashauri maafisa ugani namna ya kukabiliana na ugonjwa ama viashiria vya ugonjwa wilayani, Majukumu ya ziada ni pamoja na:

  1. Kuratibu shughuli za udhibiti wa magonjwa ya mifugo na kuyakabili pale yanapojitokeza.
  2. Kusimamia ustawi wa shughuli za mifugo na afya za mifugo wilayani.
  3. Kuratibu na kusimamia uingizwaji/utowaji wa mifugo na bidhaa zitokanazo na mifugo wilayani.
  4. Kusimamia uingizwaji na utumiaji wa vifaa tiba vya mifugo vinavyotumika wilayani katika ngazi zote kwa kushirikiana na TFDA.
  5. Kupanga na kuandaa mpango wa muda mrefu na muda mfupi wa udhibiti wa magonjwa ya mlipuko kwa wanyama.
  6. Kukusanya,kutafsiri, na kutunza kumbukumbu za magonjwa ya mifugo wilayani.
  7. Kuratibu uchunguzi wa viashiria vya magonjwa na kugundua magonjwa yanayosumbua mifugo.
  8. Kuhakikisha sheria kanuni na taratibu zinazohusiana na mifugo zinafuatwa.
  9. Kushirikiana na kituo cha uchunguzi wa magonjwa ya mifugo kwa ukaribu kilichopo Iringa.
  10. Kuhamasisha Taasisi binafsi kuwekeza na kushiriki katika shughuli zinazohusiana na udhibiti wa magonjwa.
  11. Kuandaa taarifa za mwezi, robo-mwaka na mwaka zinazohusiana na afya ya mifugo na magonjwa ya mifugo wilayani.
  12. Kutekeleza majukumu mengine ya kitaaluma na utawala kama atakavyo agiza Afisa mifugo na Uvuvi wilaya.

D-AFISA MIFUGO MSIMAMIZI WA NG’OMBE WA MAZIWA NA MBUZI WA MAZIWA (SMS DAIRY)

 

  1. Kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza kwenye uzalishaji na usindikaji wa maziwa.
  2. Kuratibu na kusimamia uendelezeji wa koosafu za  ng’ombe wa maziwa na mbuzi wilayani kulingana na sera za Taifa.
  3. Kupanga na kuratibu uendelezaji uboreshaji wa ng’ombe wa maziwa na asili
  4. Kupitia mara kwa mara mtandao wa masoko  ya mazao ya maziwa wilayani.
  5. Kusisitiza na kusimamia utekelezaji wa sheria ya maziwa katika ngazi ya wilaya.
  6. Kuandaa taarifa ya maendeleo ya sekta ya maziwa ya mwezi, robo mwaka, nusu mwaka na ya mwaka kwa ngazi ya wilaya.
  7. Kufanya kazi nyingine zozote atakazoagizwa  na  Afisa mifugo na Uvuvi wa wilaya

E-AFISA MIFUGO MSIMAMIZI WA WANYAMA WADOGO 

  1. Kufanya kazi kwa ukaribu na watafiti ili kuboresha koosafu za wanyama wadogo;
  2. Kushirikiana na wadau mbalimbali kuboresha,kuendeleza wanyama wadogo
  3. Kuratibu na kusimamia upatikanaji wa takwimu za wanyama wadogo na mazao 
  4. Kuandaa ripoti za mwezi, robo-mwaka na mwaka zinazohusiana na kundi la wanyama wadogo
  5. Kukusanya na kutafsiri takwimu za mazao yatokanayo na wanyama wadogo kwa matumizi ya Taasisi na wadau wengine.
  6. Kuhamasisha wadau mbalimbali kuwekeza kwenye kundi la wanyama wadogo
  7. Kufanya kazi zingine zozote za kitaaluma na utawala kama atakavyoagiza Afisa mifugo/Uvuvi

F- MIFUGO MSIMAMIZI WA NYAMA NA NGOZI 

  1. Kuhamasisha Sekta binafsi kuwekeza katika shughuri za biashara na viwanda vya ngozi na nyama katika Halmashauri.
  2. Kusimamia sheria ya nyama ngazi ya Halmashauri
  3. Kufuatilia uzalishaji,utunzaji,ukusanyaji na upangaji wa ngozi katika madaraja
  4. Kutoa ushauri wa matumizi ya bidhaa za ngozi
  5. Kutoa ushauri namna ya kuongeza thamani ya zao la ngozi na matumizi yake
  6. Kutoa mafunzo kwa wadau wa zao la ngozi katika Halmashauri
  7. Kupitia mara kwa mara miongozo na tafsiri ya mazao ya nyama na ngozi inayotolewa kwa wilaya kutoka ngazi ya mkoa na Taifa
  8. Kuandaa bajeti ya miundo mbinu ya machinjio na mabanda ya ngozi na minada.
  9. Kusimamia sheria ya ngozi.
  10. Kuandaa ripoti za robo na mwaka za uzalishaji wa mazao ya nyama na ngozi.
  11. Kumshauri afisa mifugo na uvuvi kwa maswala ya uzalishaji na namna ya kukabiliana na changamoto za miundombinu ya machinjio,minada na masoko ya nyama na ngozi
  12.  Kutekeleza majukumu ya kiutawala na utaalamu kama utakavyo agizwa na Afisa mifugo na Uvuvi wa Wilaya.

G-AFISA- MSIMAMIZI WA SHUGHULI ZA UTAMBUZI,USAJILI NA UFUATILIAJI    WA MIFUGO.

  1. Kufanya kazi na watafiti ili kuboresha mbali za koosafu za wanyama
  2.  Kusimamia uingizwaji na uboreshaji  wa koosafu mpya za wanyama
  3. Kusajili na kusimamia sehemu/vituo vya kutolea huduma vilivyo ndani ya Wilaya
  4.  Kuandaa na kusimamia sensa ya wanyama
  5.  Kuandaa taarifa za mwezi, robomwaka na mwaka zinazohusiana na uzalishaji,na uingizwaji wa wanyama
  6. Kukusanya kutafsiri,kukadilia idadi ya wanyama na mazao yanayozalishwa wilayani
  7. Kufanya shughuli zingine za kiutumishi zitakazotolewa na afisa mifugo na uvuvi
                          

KITENGO CHA UVUVI

        A- AFISA UVUVI (W)

  • Kusimamia  shughuli zote za uvuvi
  • Kuratibu na kusimamia utoaji wa  elimu na mafunzo kwa wataalam na wafugaji
  • Kusimamia na kutoa  vibali au leseni za uvuvi
  • Kutafsili miongozo, sheria na kanuni zinazohusiana na uvuvi
  • Kusimamia  sera ya uvuvi
  • Kusimamia na kudhibiti  viumbe vya majini na rasilimali za maji pamoja na mazingira yake
  •  
  • B-AFISA- MSIMAMIZI WA VIUMBE VYA MAJINI (AQUACULTURE)
  • Kuhamasisha  uanzishwaji  wa ufugaji  wa viumbe katika maji
  • Kutoa  elimu ya ufugaji wa viumbe vya majini (mfano samaki...)
  • Kusimamia sheria,  taratibu na kanuni za ufugaji wa viumbe vya majini
  • Kupitia na kuidhinisha maombi ya uanzishwaji wa miradi ya ufugaji wa viumbe vya majini.
  • Kukusanya, kuandaa na kuifadhi kumbukumbu za ufugaji wa viumbe majini.

C-AFISA-MKAGUZI WA SAMAKI (FISH INSPECTOR)

  • Kukagua  samaki  na mazao yake kabla ya kuingia sokoni na kwa mlaji
  • Kusimamia na kukagua  vibali vya wauzaji wa samaki sokoni na katika maduka ya samaki.
  • Kutoa maelekezo au adhabu pale ambapo taratibu za uuzaji wa samaki zimekiukwa
  • AFISA UGANI NGAZI YA KATA NA KIJIJI
  • Mtaalamu huyu anasimamiwa na Mtendaji wa Kata au kijiji lakini ata wajibika kwa Afisa mifugo na Uvuvi kama kuna swala la kitaalamu linajitokeza katika kata /kijiji chake
  • Kuhamasisha na kusimamia uundwaji wa vikundi na ushirika wa wafugaji ndani ya kata na kijiji
  • kuhamasisha na kuendesha mikutano na majukwaa ya wafugaji kwa kushirikiana na viongozi wa wananchi kama diwani,mwenyekiti wa kijiji,vitongoji na balozi walioko kwenye eneo husika kubainisha changamoto na fursa zilizopo kwenye kata na kijiji
  • kuandaa bajeti na matumizi yatakayolenga shughuli za  uzalishaji ngazi ya kijiji na kata na kuziwasilisha wilayani
  • kushirikiana na watafiti kufanya utafiti  na majaribio ya shughuli  zinazohusiana na sekta ya uzalishaji kama kilimo,mifugo na uvuvi kwa maendeleo ya kata na kijiji
  • Kushirikiana na watafiti,kampuni na taasisi mbalimbali katika kuanzisha mashamba darasa ya mifugo na samaki
  • Kubaini uwepo wa magonjwa ya mifugo na kutoa suruhisho  na ikiwa hawei kujua aina ya ugonjwa anapaswa kuripoti kwa Afisa mifugo na Uvuvi Wilaya ili yeye atoe mtaalam wa kuhakiki  na kukabili tatizo husika.
  • kuandaa takwimu za mifugo (idadi ya mifugo,mazao yanayozalishwa kama vile nyama,Maziwa,ngozi,mayai ,samaki na kiasi kinachopelekwa sokoni)
  • kuandaa taarifa ya shughuli zinazofanyika na kupeleka ripoti kwa Afisa mifugo na uvuvi .
  • kuwatambua watoa huduma za mifugo,na uvuvi kama vile wagani kazi,maduka ya pembejeo yaliyopo kwenye kata na kutoa taarifa kama kuna ukiukwaji wa taratibu za kisheria zinazohusika na huduma inayotolewa.
  • Ataandaa taarifa kutoka kwa wagani kazi, makampuni na Taasisi zinazofanyika katika ngazi ya kata na kijiji.

Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE SEMINA NAFASI YA WAANDISHI WASAIDIZI NA BVR December 19, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA AKIBA NAFASI YA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI December 19, 2024
  • TANGAZO BARAZA LA MADIWANI April 27, 2021
  • TANGAZO LA AJIRA ZA MKATABA June 10, 2021
  • Onesha Vyote

Habari Mpya

  • BLAC MAENDELEO YAHITIMISHA MAFUNZO KWA WAKAZI WA WILAYA YA RUNGWE

    May 02, 2025
  • CHANJO YA POLIO KUTOLEWA MEI MOSI

    April 16, 2025
  • KAMATI YA SIASA YAPONGEZA MIRADI

    April 15, 2025
  • MIKOPO YA ASILIMIA KUMI YAWANUFAISHA WANANCHI

    April 07, 2025
  • Onesha Vyote

Video

Vivutio vya Utalii
Picha Mjongeo Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
  • TAMISEMI

Vinganishi Linganifu

  • OR TAMISEMI
  • Wizara ya Elimu na Ufundi
  • Sekretarieti ya Ajira Utumishi wa Umma

Kipimo cha Wateja Duniani

world map hits counter

Wateja Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB

    Sanduku la Posta: Box 148

    Simu: 025 255 2586

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Huruhusiwi
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa