Idara ya Fedha inashirikiana na Idara ya Mipango kuandaa makisio ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha;
Kusimamia na kudhibiti mfumo wa kifedha na kutunza nyaraka na kumbukumbu za fedha;
Idara ya Fedha inaandaa taarifa zote za fedha zinazohusu mapato na matumizi ukilinganisha na bajeti na kutoa ushauri wa mapato na matumizi kutokana na taarifa hizo;
Kuandaa mezania ya hesabu za mwaka wa fedha husika na taarifa zingine za fedha zinazohitajika kwa Waheshimiwa Madiwani;
Kuhakikisha mfumo wa ndani wa ki-hasibu (Internal Control) unafanya kazi, kusimamia sheria, kanuni na taratibu zote za fedha;
Kusimamia na kutunza mali za Halmashauri na mifumo ya kielektroniki ya mapato na matumizi (EPICOR).
Kitengo cha Biashara:
Kuratibu utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu za sekta za Viwanda, Biashara na Masoko katika Mamlaka za Serikali za Mitaa;
Kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wafanyabiashara wadogo walioko katika sekta binafsi katika eneo lililo chini ya mamlaka ya serikali za mitaa.
Kupokea, kuchambua na kuunganisha taarifa za uzalishaji katika sekta ya Viwanda, Biashara na Masoko na kutoa taarifa OWM-TAMISEMI, Wizara ya Viwanda na Biashara na kwenye Sekretarieti za Mikoa na kushauri ipasavyo;
Kushauri na kuratibu shughuli za usajili wa shughuli za biashara katika Mamlaka za Serikali za Mitaa (Business Activities Registration) kwa mujibu wa sheria;
Kupendekeza namna ya kuboresha mazingira wezeshi ya biashara kwa madhumuni ya kurahisisha taratibu za kuanzisha biashara nchini na kushauri namna ya kuikuza Sekta Binafsi kwa lengo la kuifanya ya ushindani;
Kuwasiliana na Wizara/Taasisi na Mashirika yanayosimamia sheria/kanuni za kufanya biashara ili kupata takwimu kwa ajili ya kutathimini mwenendo wa biashara;
Kutoa ushauri juu ya mifumo ya kuwakinga wakulima na madhara ya mabadiliko ya bei (community price risk management) kama vile mfumo wa Stakabadhi Ghalani na kuhakikisha unapanuliwa kwa mazao yanayozalishwa na wakulima katika Wilaya na kuinua kipato cha wakulima;
Kuratibu maendeleo ya biashara ndogo, kati, kubwa na sekta isiyo rasmi na kutoa taarifa OWM-TAMISEMI, na Wizara ya Viwanda na Biashara na uwekezaji.
Kutoa mapendekezo ya kuboresha Sera za sekta za Viwanda, Biashara na Uwekezaji katika ngazi ya Mamlaka za Serikali za Mitaa na kuratibu mikutano ya kisekta kwa kushirikiana na wizara OWM-TAMISEMI or Mkoa.
Kutoa ushauri ya dhana ya wilaya moja zao moja (one village one product concept) kulingana na fursa zilizopo kwa kuzingatia ushindani wa soko (comperative and competitive advantage katika mamlaka za serikali za mitaa.
Kutathimini mwenendo wa biashara kwa kuangalia hali ya masoko ya ndani na nje ya nchi na kuandaa chati ya kuonyesha hali ya biashara kwa kipindi cha robo, nusu na mwaka.