23/11/2018
SOKO LETU, GULIO LETU
Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ina masoko na magulio makubwa ambayo yapo katika kata mbalimbali katika Wilaya ya Rungwe.
Masoko ambayo ni ya kudumu na yanayotoa huduma kila siku ni soko la Tandale, Soko kuu la Tukuyu mjini , soko la Kiwira na soko la Ushirika lililopo Kata ya Mpuguso.
Aidha yapo masoko mengine yajulikanayo kama magulio au Lembuka ambayo hufanyika kwa siku tofauti za wiki katika kata za Halmashauri ya Wilaya Rungwe. Magulio hayo ni Soko la Lembuka Kiwira, Soko la Tandale, Soko la Ikuti, Soko la K.K (Kyimo), Soko la Igembe Kata ya Lufingo na Kata ya Lupepo Soko la Lugombo ambapo magulio hayo hufanyika kwa siku tofauti za wiki. Wakulima na wafanya biashara kutoka sehemu mbalimbali hufanya biashara katika Masoko (Magulio) hayo.
Aidha katika masoko na magulio yote hayo hufanyika biashara za mazao ya chakula, mifugo, uvuvi, misitu na bidhaa zinazozalishwa viwandani. Bidhaa hizo hutumika ndani ya Wilaya na nyingine kwenda nje ya Wilaya, nje ya mkoa wa Mbeya na hata kwenda Nchi jirani za Malawi na Zambia.
Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Kupitia Masoko na Magulio, inanufaika na ukusanyaji wa ushuru na tozo mbalimbali kupitia Magulio na Masoko hayo. Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe imeweza kujenga miundo mbinu rafiki na wezeshi ili kuweza kufikia Magulio na Masoko hayo kiurahisi. Pia Halmashauri imefanikiwa kujenga Ghala baridi (Cold-room) katika Kata ya Kyimo eneo la Ilenge na ina mpango wa kujenga Soko Ndizi la kimataifa katika eneo hilo. Ghala hilo litasaidia kutunza bidhaa za matunda ili yaweze kusafirishwa kwenda ndani ya Nchi na Nje ya Nchi bila kupoteza ubora wake.
SOKO LA GULIO (LEMBUKA) TANDALE
Picha za wafanyabiashara na bidhaa mbalimbali katika Gulio la Tandale.(picha zote na Suzan Mhoja)
14/10/2018
MFUKO wa Maendeleo ya jamii (TASAF) katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya jumla kaya 6,132 zilizoingizwa kwenye Mpango wa kunusuru kaya Maskini tangu mpango huo uanze mwaka 2015 ili wanufaike. Mpaka sasa jumla ya walengwa 6,047 ndio wanaonufaka wa mpango huu kwani kuna baadhi ya wanufaika walifariki na wengine kuondolewa kwenye mpango huo. Wafuatao ni baadhi ya wanufaika wa mpango ambao wameelezea mafanikio yao tangu kujiunga na mpango huu.
Kwa maelezo zaidi soma hapa chini;
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa