15/10/2018
MKURUGENZI MTENDAJI HALMASHAURI WILAYA YA RUNGWE ATAMBUA UMUHIMU WA SKAUTI.
Skauti wilayani Rungwe wapewa zawadi na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Rungwe
Bi.Loema I.Peter, baada ya kuwa washindi katika mashindano mbalimbali ya kimkoa na Kitaifa.
Kimkoa walipata ushindi wa nafasi ya Kwanza baada ya kushiriki shindano la huduma za afya ya mama na mtoto lililofanyika katika uwanja wa Skauti mjini Mbeya tarehe 24 hadi 26/6/ 2018, ambapo kitaifa walishinda nafasi ya pili katika shughuli za utunzaji mazingira na mashindano hayo yalifanyika mjini Morogoro tarehe 17 hadi 23 /8/ 2018.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe alitoa pongezi hizo akiwa na baadhi ya waheshimiwa Madiwani, na Watumishi walio katika makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe tarehe 15/10/2018 katika viwanja vya ofisi ya Mkurugenzi.
Mkurugenzi Mtendaji alishukuru uongozi wa Skauti Wilaya ambao umeonyesha ushirikano mkubwa katika shughuli mbalimbali za ujenzi wa Taifa pamoja na kushiriki katika Shughuli za Kitaifa kama mapokezi ya Ugeni na Viongozi wa Kitaifa, Mbio za Mwenge wa Uhuru,utunzaji wa Mazingira ikiwa ni kupanda miti maeneo mbalimbali ya Halmashauri ya Rungwe,Kufanya Usafi katika taasisi za serikali,kuzima na kuzuia moto katika hifadhi za mlima Rungwe.
Zawadi hizo ni vyeti vya pongezi na kuthamini shughuli zao katika Halmashauri ,pamoja na fedha ambazo zilichangwa na baadhi ya watumishi katika Halmashauri ikiwa kama ni pongezi na shukrani.
Zifuatazo ni picha mbalimbali za matukio ya hafla ya kupokea zawadi na pongezi.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa