MUUNDO WA IDARA YA UJENZI NA MAJUKUMU WAHANDISI WATENDAJI (EXECUTIVE ENGINEERS)
Mhandisi Mtendaji Ujenzi (Executive Civil) daraja la II
Atafanya kazi chini ya uangalizi wa Mhandisi aliyesajiliwa (Professional engineer) na bodi ya usajili ya wahandisi ili kupata uzoefu unaotakiwa.
Kufanya ukaguzi wa barabara, madaraja na majengo mbalimbali
Kuchunguza vyanzo vya ajali barabarani.
Kufuatilia utekelezaji wa sheria na kanuni za ujenzi wa barabara na majengo
Kutayarisha bajeti ya mwaka ya ujenzi na matengenezo ya barabara, madaraja na majengo.
Kusimamia na kuratibu kazi za Barabara/Madaraja na majengo zinazotolewa na Makandarasi.
Mhandisi Mtendaji Ujenzi (Executive Civil) daraja la I
Kutoa ushauri na usimamizi wa kazi za ujenzi wa miradi ya barabara/madaraja na majengo.
Kutayarisha taarifa za maendeleo ya miradi za mwezi, robo mwaka, nusu mwaka na mwaka mzima ili kueleza maendeleo ya kazi za ujenzi wa barabara, madaraja, nyumba ikijumuisha miradi iliyokamilika na inayoendelea.
Kusimamia utekelezaji wa sheria, kanuni za barabara/madaraja na majengo na kuchukua hatua dhidi ya ukiukwaji.
Kusimamia utekelezaji wa miradi ya ujenzi na matengenezo ya barabara, madaraja na majengo.
Kutayarisha taratibu za ununuzi na kuandaa mikataba kwa ajili ya usanifu, ukarabati na kuinua viwango vya ujenzi wa barabara/madaraja na majengo.
Kutayarisha mipango ya mwaka pamoja na bajeti ya ujenzi na ukarabati wa barabara, madaraja na majengo.
Mhandisi Mtendaji Mkuu Ujenzi (Principal Executive Engineer Civil) daraja la II
Kutathimini utekelezaji wa sera na sheria za kujenga, kukarabati barabara, madaraja na majengo.
Kufanya uchambuzi wa kina wa taarifa na takwimu za kujenga/ kukarabati barabara, madaraja na majengo.
Kubuni, kusimamia na kuratibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwenye sekta ya ujenzi wa barabara, madaraja na majengo.
Anaweza kuteuliwa kuongoza Idara kwenye Wizara.
Mhandisi Mtendaji Mkuu Ujenzi (Prinzipal Executive Engineer Civil) daraja la I
Kusimamia maendeleo ya taaluma ya kiuhandisi katika sekta ya ujenzi wa barabara na mipango.
Kutoa ushauri kuhusu sera ya sekta ya ujenzi na ku………( review), sera, sheria na kanuni zake.
Kusimamia mfumo wa sheria ya sekta ya ujenzi pamoja na kanuni na taratibu kwa nia ya kuboresha ujenzi wa barabara, madaraja na majengo.
Kuratibu na kushauri mfumo wa matumizi bora ya barabara, watembea kwa miguu na wanaoendesha magari ili kuzuia ajali za barabarani.
Kusimamia utekelezaji wa makubaliano ya mikataba inayoihusisha serikali katika masuala ya ujenzi wa barabara na majengo.
Mtumishi wa ngazi hii anaweza kuongoza Idara.
Mafundi Sanifu Ujenzi (Civil Technicians)
Fundi Sanifu Ujenzi Daraja la II
Kufanya kazi za ujenzi wa kuta za nyumba na kupaka rangi na kufunga mabomba.
Kuchonga vifaa vya nyumba za serikali ikiwa ni pamoja na samani “furniture”
Kufanya kazi za upimaji (survey) wa barabara,, majengo na mifereji kama atakavyoelekeza.
Kuwapangia kazi mafundi sanifu wasaidizi na kuhakikisha wanamaliza kazi iliyopangwa.
Fundi sanifu Ujenzi daraja la I
Kufanya kazi za ujenzi wa nyumba za serikali, barabara na makalavati
Kusimamia ujenzi wa miradi ya barabara, majengo na madaraja unaofanywa na wakandarasi wadogo wadogo.
Kusimamia mafundi wa vikosi vinavyokarabati nyumba za serikali na barabara.
Kufanya makisio ya gharama na vifaa vya miradi midogo midogo.
Fundi sanifu ujenzi Mwandamizi
Kufanya ukaguzi wa ujenzi wa majengo ya serikali na barabara
Kuandaa ripoti za utekelezaji wa miradi na kiwango kilichofikiwa kwa kila kipindi cha miezi mitatu.
Kuandaa makisio ya gharama ya matengenezo ya majengo, barabara na madaraja kwa kila mwaka.
Kuandaa “Action plan” na kuhakikisha inafuatwa na walio chini yake.
Fundi Sanifu Ujenzi Mkuu
Kuratibu kazi zote zinazofanywa na wale waliopo chini yake;
Kuhakikisha kwamba shughuli za miradi ya majengo, barabara na madaraja zinatekelezwa kama ilivyopangwa.
Kutayarisha mpango mzima wa gharama za miradi yote na kushauri uongozi wa juu ipasavyo:-
Kuratibu utekelezaji wa miradi kulingana na michoro waliyopewa kutumia na endapo upo utata atashauri uongozi wa juu ili kufanya mabadiliko kurahisha utekelezaji wake.
Kufanya kazi nyingine kama atakavyopangiwa
Mafundi Sanifu Ufundi na Umeme (Mechanical & Electrical Technicians)
Fundi sanifu ufundi na umeme daraja II
Kufanya ukaguzi wa ubora wa magari ya serikali na kurekebisha ipasavyo
Kufanya upimaji wa mitambo na umeme kufuatana na maelekezo ya mhandisi.
Kufanya kazi ya kutengneza mitambo, magari na vifaa vya umeme
Kufanya usanifu wa miradi midogo midogo ya umeme, kusimamia jinsi ya kufunga mashine mpya zinazowekwa kwenye karakana za ufundi na umeme.
Fundi Sanifu Ufundi na Umeme daraja I
Kufanya makisio ya gharama na vifaa kwa miradi midogo midogo ya ufundi na kuweka umeme kwenye nyumba za serikali.
Kuongeza mafundi katika kazi kwenye karakana “Mechanical and Electrical” kufanya matengenezo ya mara kwa mara ya umeme kwenye nyumba za serikali.
Kuendeleza miradi iliyokamilika na kufanya matengenezo ya magari majokofu na viyoyozi.
Kufanya ukaguzi wa matengenezo ya mitambo, magari n.k.
Fundi Sanifu Ufundi na Umeme Mwandamizi.
Kuandaa ripoti za utekelezaji ili kujua kiwango kilichofikiwa, kwa kila kipindi cha miezi mitatumitatu.
Kuandaa makisio ya gharama ya mahitaji ya vipuri kwa ajili ya matengenezo ya mitambo, magari na vyombo vya umeme.
Kuandaa “action plan” na kuhakikisha inafuatwa na walio chini yake
Fundi sanifu Ufundi na Umeme Mkuu
Kuratibu kazi zote zinazofanywa na wale waliopo chini yake.
Kuhakikisha kwamba shughuli za matengenezo ya mitambo, magari na vifaa vya umeme inatekelezwa kama ilivyopangwa.
Kutayarisha mpango mzima na gharama za matengenezo na kushauri uongozi wa juu ipasavyo.
Kuratibu utekelezaji wa matengenezo, matatizo yanayojitokeza na kushauri uongozi wa juu ili ikibidi kufanya mabadiliko kurahisisha utekelezaji wake.