Kuhamasisha upandaji wa miti ikiwa ni hatua ya kukabiliana na changamoto ya mabadiliko ya tabia nchi na kuboresha vyanzo vya maji. Miti inayooteshwa katika eneo la Ofisi Makao Makuu hutolewa kwa wananchi bure kwa ajili ya kupanda katika makazi na mashamba yao.
Kusimamia na kulinda vyanzo vya maji kwa kutoa elimu kwa wananchi juu ya uhifadhi wa vyanzo vya maji.
Kuainisha vyanzo vya maji vilivyopo ndani ya Halmashauri na kuweka mikakati ya kuviboresha vyanzo vilivyovamiwa kwa shughuli za kibinadamu. Katika vyanzo hivyo vilivyoharibika ipandwe miti rafiki na maji ikiwa ni juhudi za kuviboresha ili virudi katika hali yake ya awali.
Kupanga na kupima maeneo yanayoiva kwa maendeleo, kuandaa mipango ya urasimishaji makazi katika maeneo yaliyokuwa kiholela.
Kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi mijini na vijijini.
Kupokea na kuweka kumbukumbu za maombi ya mabadiliko ya matumizi Ardhi na umegaji wa viwanja.
Kukusanya taarifa za utafiti na mwenendo wa soko la Ardhi.
Kufanya uthaminishaji wa mali za serikali na watu binafsi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu kusimamia.
Kusuluhisha migogoro ya ardhi, kutafsiri na kusimamia sheria za Ardhi na Mipango miji.
Kusimamia uhifadhi wa mazingira pamoja na kusimamia matumizi endelevu ya rasilimali maji, misitu, na wanyamapori kwa ajili ya faida ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho.
Pia sekta hii ipo katika mstari wa mbele katika kuongeza kipato cha mtu mmojammoja na mapato ya Halmashauri ya Busokelo na Taifa kwa ujumla kwa kuhamasisha na kuanzisha mashamba ya miti kwa ajili ya biashara.