Kupitia Mpango wa Serikali chini ya Wizara ya Kilimo na Mifugo @@wizara_ya_kilimo leo tarehe 10.1.2026 wafugaji katika kata ya Lufingo kijiji cha Kalalo wametambulishwa Mpango wa KOPA ng'ombe LIPA ng'ombe ambapo katika kata hii kwa hatua ya mwanzo jumla ya vijiji viwili vitanufaika
Vijiji hivyo ni pamoja na Kalalo na Itete ambapo jumla ya ngombe 43 watapatiwa wanufaika
Wanufaika watajiunga katika vikundi/ Ushirika ambapo itakuwa rahisi kuwatambua wenye sifa stahiki ya kupata ng'ombe kupitia Mkutano mkuu wa Kijiji
SIFA ZA WANUFAIKA
✓Awe na kipato cha chini,
✓Awe anapenda kufuga lakini hana Ng'ombe kwa sababu ya kipato kidogo
✓Awe na shamba la malisho
✓ Awe tayari kuhudumia mifugo
✓Awe tayari kutoa ng'ombe kwa mtu mwingine
✓Awe tayari kushiriki mafunzo ya shamba darasa kwa zaidi ya asilimia 95%
✓Awe tayari kuuza maziwa kupitia kikundi na chama cha Ushirika
Aidha Mradi huu utawezesha Maabara kwa ajili ya kupima afya ya mifugo, Vifaa vya usafiri na vipimo kwa Maafisa mifugo, na mengine mengi
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa