Kuwakilisha Wizara ya Elimu, Sayansi n teknolojia nat katika ngazi zote
Kufafanua na kusimamia utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo, Sheria na Kanuni katika Elimu ya Watu Wazima na Ufundi Stadi.
Kutoa ushauri wa kitalaamu kwa Halmashauri ya Wilaya, Mji au Manispaa kuhusu masuala yote ya kielimu.
Kudhibiti matumizi ya fedha za elimu kwa mujibu wa miongozo ya fedha za Serikali.
Kushughulikia upanuzi wa Elimu katika ngazi ya Elimu ya Awali, Elimu ya Msingi, Elimu ya Sekondari, Mafunzo ya Ualimu, Elimu ya Watu Wazima na Vituo vya Ufundi Stadi.
Kufuatilia kwa madhumuni ya kutathmini maendeleo ya Elimu katika Wilaya.
Kutayarisha na kusimamia utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya Elimu kila mwaka.
Kuhakikisha kwamba shule zote zinaboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.
Kuhimiza udhibiti wa nidhamu ya walimu na wanafunzi wilayani.
Kusimamia maslahi ya walimu.
Kuratibu na kusimamia mitihani ya Darasa la Nne, Darasa la Saba , Kidato cha Nne, Kidato cha Sita, Mafunzo ya Ualimu na Mitihani ya Vituo vya Ufundi Stadi katika wilaya kwa kushirikiana na Uongozi wa Elimu Mkoa na Baraza la Mitihani la Tanzania .
Kufuatilia Utekelezaji wa taarifa za Ukaguzi wa Shule na Vyuo.
Kusimamia Maendeleo ya Taaluma katika wilaya.
Kukusanya, kuratibu na kuchambua takwimu za elimu katika Wilaya kwa ajili ya Mipango ya Maendeleo katika ngazi ya Shule, Wilaya, Mkoa na Taifa.
Ni Katibu wa Kamati ya elimu na Utamaduni ya Halmashauri ya Wilaya/Mji/Manispaa kufuatana na kifungu cha 2 cha Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 na kurekebishwa mwaka 1995.
Kufanya kazi nyingine kama utakavyoelekezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya.
TAALUMA:
Kufuatilia na kusimamia utekelezaji wa taarifa za ukaguzi wa shule za sekondari.
Kuratibu na kusimamia mitihani ya kitaifa inayoendeshwa kwa shule za Sekondari katika Halmashauri.
Kubuni mipango ya mitihani ya elimu ya sekondari na kusimamia utekelezaji wake.
Kuhakikisha kuwa walimu na watumishi wengine wa shule za sekondari wanafanyiwa tathmini ya wazi ya utendaji kazi (Open Performance Review and Appraisal System) – OPRAS
Kubuni na kuratibu mipango ya mafunzo kazini kwaa walimu na watumishi wengine wa shule za Sekondari.
Kuratibu mashindano ya michezo na taaluma ya Shule za sekondari katika Halmashauri.
Kusimamia maendeleo ya taaluma na michezo ya shule za sekondari katika Halmashauri.
Kuhakikisha walimu wa Shule za sekondari wanapangiwa katika shiule kwa kuzingatia ikamainayokubalika.
Kufanya kazzi nyingine nitakazopewa na Mkurugenzi wa Halmashauri au Afisa Elimu wa Elimu ya Sekondari wa Halmashauri.