Naibu Katibu Mkuu (Elimu) OR-TAMISEMI Bwana Tixon Nzunda alifanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe tarehe 24/01/2019. Katika Ziara hiyo alitembelea shule ya sekondari ya wasichana Kayuki yenye kidato cha kwanza mpka kidato cha sita akiwa ameongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Bi.Loema Peter pamoja na wakuu wa idara mbalimbali katika Halmashauri.
Katika ziara hiyo aliweza kutembelea mindo mbinu ya shule hiyo iliyo jengwa kwa fedha za P4R- ambazo ni fedha zinazotolewa na Serikali kuu,Shule ilipokea kiasi cha fedha 259,000,000/= kwaajili ya ujenzi wa miundo mbinu ya kidato cha v katika shule hiyo. Fedha hizo hutolewa kwa shule zinazofanya vizuri katika mitihani ya kitaifa. Miundo iliyo katika shule hiyo ni vyumba 4 vya madarasa, chumba 1 cha ofisi ya walimu, ukarabati wa daharia 3, ujenzi wa vyoo vya matundu 17 na maabara 3.
Aidha katika ziara hiyo pia aliongea na walimu pamoja na wanafunzi wa shule hiyo baada ya kupokea taarifa ya shule iliyosomwa na Mkuu wa Shule hiyo Bi Bertha M. Sarufu ilieleza mambo mbalimbali ya shule hiyo ikiwa ni pamoja na maendeleo ya kielimu ya shule hiyo ambapo kwa matokeo ya mfulilulizo kwa miaka mitatu ya karibu kwa akidato cha ii na kidato cha iv Kwa kidato cha pili matokeo yalikuwa ni kama yafuatayo 2016 - 100%, 2017 -99.4%,2018 -100% na kwa kidato cha iv matokeo yalikuwa 2016 -95.7%, 2017 - 98.6% na 2018 -100%.
Pamoja na taarifa hizo za matokeo zipo changamoto ambazo zilisomwa katika taarifa hiyo ikiwa ni upungufu wa waalimu wa sayansi,maji,maktaba,ukumbi na viwanja vya michezo Katika changamoto hizo ambazo Naibu Katibu Mkuu alizo ahidi kuzifanyia kazi ni kupatikana kwa maktaba ambapo alisema kwa mwaka ujao wa fedha atahakikisha shule hiyo inapata maktaba kwa kuleta fedha kutoka OR_TAMISEMI. Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Rungwe alieleza kuwa tayari alitenga kiasi cha tsh.20,000,000/= kwaajili ya ufanisi wa upatikanaji wa maji katika shule hiyo.
Aidha wadau wa elimu mbalimbali nao wanashiriki vizuri katika kuendeleza elimu katika shule hiyo ambapo kampuni ya Mohamed Enterprises walitoa heka 20 za ardhi iliyo jirani na shule hiyo ambazo zitatumika kujenga (miundo mbinu) maktaba, ukumbi, na viwanja vya michezo.
Baada ya kupokea taarifa aliongea na wanafunzi kwa kuwasisitiza kuongeza zaidi bidii katika masomo yao na kufuta kabisa daraja 0 na ikiwezekana na daraja La 4 katika shule hiyo. Pia aliwapongeza sana kwaufaulu mzuri kwa miaka mitatu mfululizo na pia aliwapongeza zaidi walimu na uongozi wote wa shule pamoja na bodi ya shule kwa usimamizi mzuri wa shule.
Furaha ilizidi zaidi baada kupata taarifa ya matokeo ya kidato cha iv ya mwaka 2018 ambayo yalitangazwa baada ya Naibu Katibu Mkuu kuondoka shuleni hapo ambapo kwa shule hiyo haikua na daraja 0. Hivyo ikawafanya walimu na wanafunzi hao kufurahia kuanza kufuta daraja la 0 (sifuri) katika shule hiyo. Aidha katika matokeo haya Wilaya ya Rungwe imekua nafasi ya tatu kimkoa na nafasi ya 28 kitaifa.
Pia alimtaka Mkuu wa shule kuendelea na usimizi huo mzuri na kutekeleza mikakati waliyojiwekea kwaajili ya kuinua zaidi elimu shuleni hapo.
Shule ya sekondari ya wasichana Kayuki ilianzishwa mwaka 2004 kwa kidato cha i -iv na ilipofika 2017 ilianzishwa kidato cha v kwa tahasusi za PCB na CBG mpaka sasa shule ina kidato cha i -vi kwa jumla ya wanafunzi 986 na walimu 32.
Baada ya kutoka shuleni hapo Naibu Katibu Mkuu alielekea katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Msasani ambako alifanya kikao na wakuu wa idara za Halmashauri za Wilaya Rungwe na Busokelo, Wakuu wa Shule za Sekondari ,Walimu wakuu shule za msingi, Waratibu Elimu Kata wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe. Katika kiako hicho aliwasisitiza watumishi hao kufanya Nazi kwa juhudi ili kuinua na kuboresha elimu.
(pichani:Picha ya kwanza ni Naibu Katibu Mkuu akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Ndg.Julius Challya na Viongozi wa Ofisi ya Mkoa wa Mbeya na Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe.
Picha nyingine ni wanafunzi na walimu wa sekondari ya wasichana Kayuki wakiwa katika matukio mbalimbali katika ziara ya Naibu Katibu Mkuu _Elimu OR _TAMISEMI )
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa