Makandana Hospitali
Msafara Mwenge wa uhuru wilayani Rungwe umetembelea na kukagua ujenzi unaoendelea wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika hospitali ya Wilaya ya Rungwe, Makandana.
Mwenge wa Uhuru umeweka Jiwe la Msingi katika Jengo hili la ghorofa Mbili.
Kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa Wilaya ya Rungwe Dr Diocles Ngaiza ameeleza kuwa ujenzi huo unatarajia kugharimu kiasi cha shilingi cha zaidi ya shilingi bilioni 2 mpaka kukamilika kwake .
Jengo hili litakapokamilika linatarajiwa kuongeza ubora wa huduma hasa kwa mama na mtoto
Aidha Dr Ngaiza ameishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutenga fedha kwaajili ya ujenzi wa hospitali hii kongwe katika wilaya ya Rungwe
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa