Ziara ya mkurugenzi mtendaji halmashauri ya wilaya ya Rungwe Bibi Loema Peter imefanyika kwa kutembelea shule zote za kidato cha sita wilayani Rungwe huku akisisitiza mambo yafuatayo kuelekea mtihani wa Taifa/NECTA mwezi huu.
1.Wanafunzi wanahitajika kujiamini na kusoma kwa bidii ili kujitwalia matokeo mazuri.
2. Wanafunzi waendelee kujiandaa na kuondoa hofu dhidi ya CORONA huku wakichukua tahadhari zote.
3. Wanafunzi waendelee kuwa na nidhamu kwani kushindwa kufanya hivyo watashindwa kufaulu mitihani yao.
4. Walimu wafundishe kwa bidii muda wote huku wakirejea maeneo maalumu ya mkazo kuelekea mtihani wa taifa.
5.Wanafunzi waendelee kufuatilia vipindi vya masomo kupitia Televisheni kwa lengo la kujiongezea maarifa.
6. Mwanafunzi akipata daraja la sifuri, au la nne atakuwa ameikosesha furaha nafsi yake, na taifa kwa ujumla na hivyo kuleta takwimu mbaya kiwilaya.
7. Vipindi vifundishwe hadi usiku na hasa inapowezekana kufidia muda uliopotea hapo awali wakati wa likizo.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa