Kilimo cha zao la Vanila katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe kimeendelea kushika kasi.
Miaka mitatu tangu zao hili liasisiwe Wilayani hapa matunda yameanza kuonekana.
Mboka Mwakatumbula mkazi wa kata ya Kyimo anaeleza kuwa juhudi, maarifa na ufuatiliaji wa namna bora ya uzalishaji wa Vanila umesaidia kufikia kiwango kizuri Cha uzalishaji wa zao hilo.
Vanila ambayo hustahimili katika joto la wastani wa sentigredi 25- 35 , Mwinuko wa Mita 1000- 1500 kutoka usawa wa Bahari na mvua ya Wastani wa Millita 2500-5000 kwa mwaka imepelekea kata ya Kyimo, Ikuti, Bagamoyo, Kinyala, Iponjola, Nkunga, Malindo, Suma, Masoko, Kisondela, Msasani, Makandana, Lufingo kunufaika na zao hili.
Bwana Juma Mzara Mtalaamu wa mazao katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ameeleza kuwa mpaka Sasa zaidi ya miche 61,000 imepandwa na kuwafikia wakulima 1000 huku lengo likiwa ni kuwafikia wakulima wote.
Kwa Sasa vikinyo/ miche inapatikana katika kituo Cha kilimo kilichopo katika Kijiji Cha Ilenge (Sogea).
Soko kubwa la Vanila linapatikana katika nchi za ulaya, Amerika na Asia.
Bei imekuwa ikibadilika kulingana na mahitaji ya soko la dunia. Mathalani Kilo Moja mwaka 2019 iliuzwa kati ya shilingi 100,000- 150,000 kwa kilo moja.
Vanila huzalishwa zaidi katika Mkoa wa Kagera, Zanzibar, Morogoro, Kilimanjaro, Tanga na Arusha na Sasa Rungwe Mbeya.
Vanila hutumika kama kiungo na kuongeza radha katika vinywaji kama juisi, yogati, pamoja na biskuti, keki, iskrimu, na vyakula mbalimbali.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa