Kamati ya Usimamizi zahanati ya Suma iliyopo kata ya Suma imeketi leo tarehe 22.03.2023 lengo mahususi likiwa ni upatikanaji wa dawa katika zahanati hiyo, taarifa ya fedha na Mabadiliko ya kiingilio cha kumuona Mganga.
Katibu wa kikao hicho ambaye pia ni mganga Mfawidhi wa Zahanati hiyo Dr.Liberty Manyika ameeleza kuwa katika robo hii kuanzia mwezi Januari -Machi 2023 hali ya upatikanaji wa dawa katika zahanati hii imeendelea kuwa nzuri hali iliyosaidia kuimarisha afya ya jamii na kuongeza ustawi bora wa wananchi.
Aidha imeelezwa Kuwa katika kipindi hicho zahanati kiasi cha shilingi million 3,317,618.49 fedha zilizotokana na Mfuko wa bima ya afya, Malipo ya papo kwa papo, na Mfuko kabambe wa afya(HSBF).
Pamoja na mambo mengine mapato hayo yamewezesha Ununuzi wa vifaa vya usafi, kulipia ankara ya umeme, na kuwezesha shughuli za lishe, chanjo, huduma ya mkoba,
Katika hatua nyingine kikao kimeridhia na kupitisha ada ya kumuona Mganga ambapo kwa ngazi ya zahanati na Vituo vya afya itakuwa shilingi 3000/=, na Hospitali ya wilaya itakuwa 5,000/=
Awali gharama ilikuwa shilingi 8000 kwa zahanati, vituo vya afya, na hospitali ya awali hatua ya sasa itaongeza unafuu kwa wananchi na hivyo kumudu matibabu.
Mabadiliko haya yataanza kutekelezwa kuanzia tarehe 01 Aprili 2023 katika maeneo yote ya kutolea huduma ya afya katika Halmashauri ya wilaya ya Rungwe.
Aidha kikao hicho pia kimehudhuriwa na wajumbe kutoka Mpango wa Uimarishaji utawala bora na Ushirikishwaji wa wananchi (PS3) ambapo kikao kimeshauriwa yafuatayo:
✓Kuhakikisha taarifa ya mapato na matumizi inasomwa kila robo na kubandikwa kwenye mbao za matangazo katika zahanati, sokoni, maeneo ya ibada, ofisi ya kata, vijiji na vitongoji.
✓Kuimarisha mifumo ya ukusanyaji mapato sambamba na utoaji huduma bora kwa wananchi
✓Ushirikishwaji wa wananchi katika mipango ya maendeleo ya zahanati yao.
✓ Kuwahamasisha wananchi kujiunga na kutumia bima ya afya ya Taifa na ile iliyoboreshwa (NHIF&ICHF) ili kuwapunguzia gharama ya matibabu na kuongeza mapato ya zahanati.
Kikao hicho kilichohudhuriwa pia na Katibu wa afya Mkoa wa Mbeya Bi.Hobokela Mwimbe kimejumuisha wajumbe sita kutoka vijiji vya Kituli, Suma, Busona na Malamba pamoja na Mtendaji wa kata hiyo.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa