Kituo cha afya kilichopo katika kijiji Swaya kata ya Swaya Halmashauri ya wilaya ya Rungwe inatatarajiwa kuanza kutoa huduma za afya hivi karibuni baada ya ujenzi wake kukamilika.
Kituo hicho kilianza kujengwa mwaka 2016 kwa ushirikiano wa wananchi na Serikali umegharimu zaidi ya shilingi million 50.
Kukamilika kwake kutaharakisha huduma za afya kwa wakazi wa kijiji hiki hasa huduma ya mama na mtoto ambayo wamekuwa wakiipata vijiji vya jirani na hivyo kutishia uhai na afya zao.
Mbele ya kamati ya Uchumi, Fedha na Mipango (FUM), Serikali ya Kijiji Imeeleza kuwa ujenzi wa nyumba za wataalamu wa afya utaanza hivi karibuni.
Mheshimiwa Mpokigwa Mwankuga ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe ambapo amesifu jitihada zinazofanywa na wakazi wa kijiji hicho katika kuchangia shughuli za maendeleo na kuomba vijiji vingine kuiga mfano huo badala ya kuacha serikali itekeleze miradi yote bila nguvu za wananchi.
" Ninawahidi kuwapa ushirikiano kila itakapowezekana ili kuhakikisha tunatekeleza ilani yetu ya Chama cha Mapinduzi kwa Vitendo" Ameongeza Mhe. Mwankuga.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa