Wanafunzi wa kike waliokatisha Masomo kutokana na sababu mbalimbali wakijiandaa kufanya jambo mbele ya mgeni rasmi katika maadhimisho ya wiki ya elimu ya Watu wazima ambapo kimkoa imeadhimishwa Leo tarehe 15.10.2022 Wilayani Kyela huku Afisa Elimu Mkoa Mwalimu Ernest Hinju akiwaagiza kusoma kwa bidii na hivyo kupata maarifa na ujuzi utakaowasaidia kuvuna rasiriamali zinazowazunguka hali itakayosaidia kuchavusha uchumi ngazi ya kaya na taifa kwa ujumla.
Katika Kituo cha mafunzo kilichopo katika shule ya Sekondari Kiwira Wilayani Rungwe kina wanafunzi 39 ambapo wanafunzi hao hufundishwa Masomo mbalimbali baada ya muda wa kawaida (jioni) kwa kutumia walimu wa shule hiyo.
Katika vituo vyote wanafunzi hao waliokatisha Masomo husoma bila gharama yeyote/ bure ikiwa ni juhudi za Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha wasichana wote wanapata elimu bila kikwazo chochote.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa