Mtendaji wa kata ya Kisondela Bi. Sara Kamagi ameishukuru Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Rungwe kwa Kumkabidhi pikipiki ikiwa ni motisha na nyenzo muhimu ya kuongeza ukusanyaji wa mapato sambamba na kuharakisha shughuli za utawala bora katika kata yake.
Bi Sara ameeleza kuwa awali walikuwa wanatumia gharama kubwa kukusanya mapato kutoka kwa watoza ushuru waliopo kona zote za kata hiyo lakini sasa itakuwa rahisi kuwafikia na hivyo kongeza ufanisi wa mapato ya serikali sambamba na kuvuka lengo walilojiwekea.
Kata zilizonufaika na pikipiki hizo ni pamoja na:
1. Msasani
2.Kisondela
3.Ndanto
4.Kiwira
Akikabidhi pikipiki hizo Mkurugenzi Mtendaji Bwana Renatus Mchau (kulia) ameomba watendaji wa kata kuzitunza na kuzitumia katika malengo yaliyokusudiwa ili kupanua wigo wa mapato na kuzuia mianya yote ya utoroshaji mapato ya serikali.
Halmashauri ya wilaya ya Rungwe inatarajia kukusanya na kutumia jumla ya Shilingi 52,636,564,958.00 kutoka vyanzo mbalimbali vya ndani na nje katika mwaka wa fedha wa serikali 2021/2022.
Mbele ya Baraza la madiwani llilioketi tarehe 30.07.2021 Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe Mhe. Mpokigwa Mwankuga alieleza kuwa katika mwaka wa fedha uliopita halmashauri imekusanya mapato ya ndani mpaka kufikia asilimia 99%, jitihada zilizooneshwa na wananchi waaminifu, watendaji kwa kushirikiana na waheshimiwa madiwani.
Aidha Halmashauri imechangia mpaka kufikia asilimia 111.6 % (imevuka lengo) kwenye shughuli za maendeleo kupitia mapato yake ya ndani hali iliyochochea uboreshaji wa huduma za kijamii katika maeneo mbalimbali sambamba na Ustawi pamoja na uchavushaji wa uchumi katika ngazi ya kaya na wilaya kwa ujumla.
Hata hivyo Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mhe. Dkt Vicent Anney ameendelea kuonya watu wanaotorosha mapato ya serikali kuwa kwa kufanya hiyo wanafifisha jitihada ya kuwaletea huduma wananchi sambamba na kuboresha miundombinu ya barabara, maji, na umeme na zingine nyingi.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa