Takribani Km 60 kutoka Uyole jijini Mbeya mpaka Tukuyu Mjini Halmshauri ya wilaya ya Rungwe inakufungulia fursa za uwekezaji na kujionea maeneo mbambali ya uwekezaji.
Rungwe inayopata mvua takribani mwaka mzima chini ya Mlima Mrefu kuliko yote Nyanda za juu Kusini ina udongo wa Kivolkano na hivyo kuwa na rutuba ya kuzalisha mazao ya Kahawa, Migomba, Parachichi, Nanasi, Kakao, Chai, Vanila, miti ya mbao, na kwa kiasi Michikichi, na korosho katika ukanda wa chini.
Hali ya hewa nzuri pia inakuwezesha kufuga ng'ombe wa maziwa na hili ni kutokana na kuwa na malisho ya kutosha na maji ya kunyweshea mifugo.
Wastani wa lita 30 za maziwa huzalishwa kila siku huku kampuni ya ASAS DAIRIES ikikusanya kiasi cha lita 20,000 kutoka kwa wafugaji.
Aidha Rungwe inavyo vivutio vingi vya utalii vikiwemo vinavyotokana na maji, misitu , utamaduni, na majengo ya kale.
Maporomoko ya maji Kaporogwe, Malasusa, Mti katembo, Malamba, Ziwa Kisiba, Ngosi na Daraja la Mungu ukifika utajionea raha isiyo kifani.
Kisiba Campsite, Isongole fishing camp na Kalongo farm and ecosystem home wakionesha mfano mzuri wa uwekezaji sekta ya utalii.
Mkurugenzi Mtendaji Halimashauri ya wilaya ya Rungwe Bwana Renatus Mchau anawaalika wawekezaji wote kuwekeza katika
Maeneo mbalimbali ya kiuchumi, na kijamii kwa faida lukuki na maendeleo ya taifa letu.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa