Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ameanza ziara leo jumapili tarehe 01.8. 2021 katika wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya kwa kutembelea Halmashauri ya wilaya ya Rungwe pamoja na Bosokelo.
Akiwa katika Shamba na kiwanda cha KUZA Afrika (Avocado) Mhe. Majaliwa amemshukuru mwekezaji kwa kujuhudi kubwa anazozifanya kuanzisha na kupanua soko la matunda ya parachichi ndani na nje ya nchi hali inayochochea wakulima wengi kuendelea kuzalisha kwa wingi zao hilo
.Aidha Mhe. Majaliwa meahidi serikali kuendelea kufungua soko la zao hilo katika mataifa mengi nje ya nchi hususani Afrika ya Kusini na bara la Ulaya ili kumpa fursa mkulima kufaidika na jasho lake na hivyo kujinasua na umasikini.
" Ndugu zangu niwambie ukweli, Parachichi linalipa, Niwaombe muwapandie watoto wenu hata heka moja tu, hii itasaidia kuwasomesha maisha yao yote katika shule mbalimbali" Ameongeza na Kusisitiza.
Awali Mbunge wa jimbo la Rungwe Mhe. Antony Mwantona ameomba vifungashio vya zao la viazi mviringo kutazamwa kwa namna nzuri kwani Lumbesa imekuwa kero na mbinu ya kumnyonya mkulima mnyonge.
Akijibu, Naibu waziri Kilimo, Mhe Hussein Bashe ameeleza kuwa baada ya ziara hii atawakutanisha wakuu wa mikoa yote inayozalisha viazi mviringo ili kutafuta namna bora ya ufungashaji na kulinda maslahi ya mkulima.
Pamoja na hayo Mhe. Bashe amearifu kuwa serikali inaandaa mkakati wa kuandaa vitalu vya miche ya maparachichi itakayogawiwa bure kwa wakulima ikiwa ni mkakati wa kukuza uwanja mpana wa uzalishaji wa zao hili.
Kampuni ya KUZA AFRIKA kwa kushirikiana na Kanisa la Moravian Tanzania ina jumla ya hekta 360 za parachichi ambapo pia hujishughulisha na usindikaji wa mafuta yanayotokana na zao hilo
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa