Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe afanya mkutano na Wauguzi na Matabibu kutoka Vituo vya Afya na waliopo Hospitali ya Wilaya ya Rungwe Leo tarehe 13/7/2018. Mkutano huo umefanyika katika uwanja wa Kliniki ya Macho hospitali ya Wilaya Rungwe Tukuyu Mjini.
Katika mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Bibi Loema I.Peter aliongozana na Afisa Utumishi Wilaya, Kaimu Mweka Hazina wa Wilaya pia walikuwepo viongozi wa hospitali ambao ni Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya,Katibu wa Afya na Wakuu wa Vitengo na Idara katika Afya.
Kero hizo ni kupanda madaraja,kubadilishiwa miundo ya kiutumishi,malimbikizo ya madai mbalimbali,posho ya sare za waaguzi,madai ya likizo,huduma za masomo,kuumia kazini, na malipo ya uhamisho,matibabu,ukosefu na kuharibika vifaa tiba,posho ya Masaa ya ziada,posho ya kuhamisha wagonjwa kutoka vituoni kwenda hospitali ya Wilaya au Hospitali ya Rufaa Mbeya.
Afisa Utumishi wa Wilaya ya Rungwe Ndugu Jumanne Chaula alijibu kero hizo za kiutumishi na Utawala kwamba kwa suala la kupanda madaraja inategemea na muda ambao mtumishi ametumikia daraja alilo nalo.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa