Katika kutambua jitihada za watumishi wa Idara ya Afya katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi, Kituo Cha Afya Kyimo wameibuka kidedea katika utoaji wa huduma bora za afya kwa wananchi ; Ambapo kwa hatua hiyo leo tarehe 29.8.2025 timu ya Usimamizi wa huduma za Afya ya Wilaya, (CHMT) imefika katika Kituo hiki na kuwapongeza watumishi kwa kazi kubwa wanazozifanya katika kutoa huduma bora kwa wananchi.
Kwa Sasa Kituo hiki kinahudumia wananchi 50 hadi 100 kwa siku huku Wajawazito 100 hadi 150 wakijifungua kwa mwezi.
Pia Kituo hiki kumeanza kupokea Rufaa za Wajawazito kwa ajili ya Upasuaji wa dharula kutoka katika vituo vingine vya tiba na kwa wastani wajawazito 20 hadi 40 wanapata huduma ya Upasuaji kwa mwezi katika Kituo hiki.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa