Watanzania wameendelea kukumbushwa kujitokeza na kushiriki kwa wingi zoezi la Sensa ya watu na Makazi linalotarajiwa kufanyika agosti 23 mwaka huu.
Wakiongea katika kipindi cha Asubuhi leo tarehe 17.06.2022 kupitia 102.5 Mhz- Rungwe FM viongozi wa dini wameomba wakazi wa wilaya ya Rungwe kujiepusha kuwaficha baadhi ya watu hasa Wenye ulemavu wa viungo kwani kwa kufanya hivyo wanainyima fursa Serikali kupanga mipango yake endelevu kwa watu wake.
Aidha wameomba wakazi wa Wilaya ya Rungwe kutohujumu zoezi hili la kitaifa ambalo litajumuisha upatikanaji wa taarifa/takwimu sahihi katika kaya zote nchini Tanzania
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa