Siku ya Mwanamke duniani leo imeadhimishwa katika Halmshauri ya Wilaya ya Rungwe.
Katika maadhimisho hayo mamia ya wanawake wamejitokeza huku wakitoa misaada kadhaa katika Gereza la Tukuyu na Shule ya msingi mchanganyiko Katumba II
Wakiwa katika Gerera la Tukuyu wameshukuru uongozi wa gereza hilo kwa huduma wanayotoa kwani kwa kufanya hivyo wanasaidia kuijenga jamii kuishi katika maadili mema.
Akikabidhi zawadi hizo Afisa maendeleo ya Jamii wilaya ya Rungwe Bibi Inonsecia Miho amesema kuwa misaada hiyo itakuwa endelevu ikiwa ni sehemu ya kipato cha wanawake wanachozalisha kila siku na kukirejesha kwa jamii wakilenga kundi lenye mahitaji maalumu kama wafungwa, watoto yatima na walemavu.
Hata hivyo Mkuu wa Gereza la Tukuyu afande Anganile Mwakalobo ameshukuru kwa msaada huo uliotukuka na kuomba kuendelea kufanya hivyo kila mara kwani wafungwa katika gereza hilo wana mahitaji endelevu na gereza kwa kushirikiana na wadau mbalimbali watasaidia kuzikwamua na hivyo kuongeza ustawi wa maisha yao ya kila siku.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa