Waziri wa Nishati Dr.Merdad Kalemani ametoa maagizo kwa watumishi wa TANESCO wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya alipokuwa katika ziara yake ya kutembelea miradi ya umeme vijijini, ambapo amewataka wawasimamie wakandarasi ili kufanikisha zoezi la usambazaji umeme kwa wananchi.
Akizungumza na wanachi mbele ya mkuu wa wilaya ya Rungwe Mh.Julius Chalya, Waziri wa Nishati Dr.Kalemani amewataka watumishi wa shirika la umeme wilayani hapa kuhakikisha wanaweka vituo kwa ajili ya kuwapatia huduma ya ulipiaji umeme katika vijiji vyao kutokana adha ya umbali wanayoipata kwenda Tukuyu mjini katika ofisi hizo.
Pamoja na hayo Dr.Kalemani ametoa maelekezo kwa wananchi juu ya gharama za kuingiza huduma hiyo ya umeme ni shilingi 27000/=. Pia aliwasisitiza watumishi wa shirika la umeme Tanzania kwa kushirikiana na wakandarasi wa umeme REA kuhakikisha kila nyumba ya wananchi inapata huduma ya umeme.
Aidha Waziri ameaagiza shirika la TANESCO kuhakikisha huduma hiyo ya umeme inapatikana hata kwa wale ambao hawajajenga ila wanamiliki viwanja wapatiwe umeme kwa kusimika nguzo katika maeneo yao huku wakisubiri kujenga nyumba katika maeneo hayo.
Hata hivyo ikumbukwe kuwa hii ni awamu pili ya Waziri huyu wa Nishati Dr.Merdad Kalemani kutembelea wilaya ya Rungwe tangu aingie madarakani kwa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Joseph Magufuli.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa