WANANCHI SIMAMIENI MIRADI KATIKA MAENEO YENU
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Rungwe Bwana Renatus Mchau amefanya ziara katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa zahanati ya Matwebe, Ujenzi wa bweni katika shule ya sekondari Masukulu, upanuzi wa zahanati ya Masoko, Kituo cha afya Iponjola , Rungwe sekondari pamoja na ujenzi wa shule Mpya Mchepuo wa Kingereza ILENGE kata ya Kyimo.
Katika ziara hiyo Bwana Mchau ameagiza mafundi wote wanaotekeleza miradi ya maendeleo kuzingatia weledi , Maarifa pamoja na Ujuzi ili ikamilike katika ubora na kwa wakati.
Aidha ameagiza mafundi wote walioshindwa kuzingatia taratibu za ujenzi kubomoa kwa gharama zao na hivyo kuepukana na tatizo la kuingiza serikali katika gharama zisizostahiki.
Amesema serikali inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan inatoa fedha nyingi kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo fedha ambazo wananchi wangechangishana mifukoni.
Kwa hatua hiyo amewakumbusha wananchi kusimamia miradi yao ipasavyo badala ya kuwaachia mafundi wakitekeleza bila usimamizi.
Aidha amesisitiza viongozi katika ngazi ya vijiji, kata, elimu na afya kuhakikisha wanasoma mapato na matumizi kwa wananchi dhidi ya Miradi ya Maendeleo ili kujenga Mazingira mazuri ya uwazi na Uwajibikaji.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa