Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ni miongoni mwa Halmashauri katika Mkoa wa Mbeya zilizoidhinishiwa kiasi cha fedha 1000,000,000.00 kutoka Serikali ikiwa ni ruzuku ya ukarabati wa vituo vya afya vya Ikuti na Masukulu kwa mwaka wa fedha 2017/2018.
Katika ujenzi na ukarabati wa vituo hivyo yamejengwa na kukarabatiwa majengo/miundombinu zaidi ya 21 ambayo yamekamilika kwa 100% na majengo yote muhimu yameanza kutoa huduma baada ya kupata na kupokea vifaa tiba.
Ujenzi na ukarabati huo wote umegharimu kiasi cha fedha tsh. 1,217,809,124.67 ikiwa ni fedha toka Serikali Kuu,Halmashauri ya Wilaya kupitia mapato ya ndani,Mfuko wa Jimbo na Michango ya Wananchi/Wadau wa Maendeleo.
Baada ya kukamilika vituo na kuanza kutoa huduma jumla ya wananchi 21,691 wa kata za Masukulu na Ikuti wananufaika kwa kupata huduma za afya zinazotolewa na vituo hivyo, aidha kuna wananchi wanaofuata huduma hizo katika kata ya Ikuti wakitokea vijiji vya jirani vya Wilaya ya Ileje.
Huduma zinazotolewa katika vituo hivyo ni huduma kwa wagonjwa wanje (OPD), huduma ya mama na mtoto, huduma ya usafi wa meno na kinywa, huduma ya wagonjwa wanaolazwa, huduma ya uzazi wa mpango, huduma ya maabara, huduma ya rafiki kwa vijana balehe, huduma ya tohara kwa wanaume, huduma ya unasihi na upimaji VVU, huduma ya kujifungua, huduma ya ushauri na lishe, huduma ya kuzuia ukatili wa kijinsia, huduma za upasuaji, huduma za kuhifadhi maiti, huduma za “X-ray na utra sound”.
Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe bado inaendelea kuboresha huduma za afya kwa kushirikiana na wananchi pamoja na wadau wa maendeleo kwa kujenga vituo vya afya ambapo mpaka sasa vituo vitatu vinaendelea kujengwa kwa kutumia nguvu za wananchi na wadau wa maendeleo; vituo hivyo vipo katika kata za Isongole, Masoko na Mpuguso.
Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe inaipongeza serikali ya awamu ya tano chini ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt John Joseph Magufuli kwa kuwezesha utoaji wa fedha hizo ambazo zimesaidia kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Picha za baadhi ya majengo ya kituo cha afya masukulu
Baadhi ya picha za majengo kituo cha afya Ikuti
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa