Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Rungwe Bwana @renatus_blas akifurahi jambo baada ya kupokea Tuzo ya Vikombe pamoja na Medali kutoka kwa Wachezaji wa Timu ya SHIMISEMITA wilaya ya Rungwe Kufuatia kufuzu michuano hii iliyofanyika mwishoni mwa mwezi August 2025 jijini Tanga
Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe imeshiriki michuano hii na kuibuka mabingwa katika nafasi mbalimbali katika fani ya Mpira wa miguu, Kikapu, Mbio, Tufe, Mkuki, handball na mingine mingi.
Awali akiwapongeza wachezaji hawa Bwana Mchau amewapongeza kwa hatua waliyofikia na kuwa kufanya hivi wameweka alama chanya kwa wilaya ya Rungwe.
Mchau ameongeza kuwa mara zote timu kutoka Rungwe imekuwa tishio katika michezo mbalimbali, na mara hii imejidhihirisha kwa kutwaa medani nyingi na vikombe mbalimbali
Pamoja na Hayo amewataka wachezaji kuendelea na maandalizi kwa ajili ya michuano hii jijini Mbeya mwakani 2026 ambapo amewawekea malengo ya kuchukua ubingwa michezo yote.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa