Mafunzo ya stadi za maisha kwa wanafunzi yamewakutanisha walimu 103 kutoka Shule za msingi , 32 kutoka sekondari na Walimu wakuu wa shule zote 149 katika shule za msingi Halmashauri ya wilaya ya Rungwe.
Mafunzo hayo yaliyolenga kuwajengea uwezo walimu kuwatambua, kuwasaidia na kuwapa mwelekeo sahihi wanafunzi na hivyo kukabiliana na mabadiliko mbalimbali ya kimwili (makuzi), kitabia na hivyo kuwa na nidhamu bora shuleni, katika jamii na hivyo kuongeza ufaulu katika masomo yao.
Akifunga mafunzo hayo Afisa Elimu Sekondari Mwalimu Yona Mwaisaka amewaomba wahitimu wa mafunzo hayo kwenda kuyatumia vizuri kwa walengwa na hivyo kuwabadilisha wanafunzi sambamba na kujenga taifa imara.
Aidha mwalimu Mwaisaka ameomba walimu kwenda kushirikiana na jamii/wazazi kutoa elimu dhidi ya stadi za maisha kwa wanafunziili kuleta usumaku imara kwa watoto na hivyo kuchavusha maarifa shuleni na nyumbani katika ngazi ya kaya.
Hata hivyo ameagiza shule zote kuanza kutoa elimu ya michezo kwa wanafunzi ikilenga kuleta uchangamshi na hivyo kuondokana na tatizo la udumavu kwa wanafunzi.Wakati huohuo mratibu wa mafunzo hayo ambaye pia ni Afisa Elimu Taaluma Mwalimu Michael Malecela ametaja madhara ya wanafunzi kukosa stadi za maisha kuwa ni pamoja na wanafunzi kupata mimba za utotoni, Kujiingiza katika vitendo viovu kama matumizi ya madawa ya kulevya na jinai zingine kadhaa, kushindwa kuchagua masomo sahihi ya kusoma kulingana na uelewa, kushindwa kuchagua taaluma sahihi ya kusomea kulingana na ufaulu wao
Mafunzo haya yamefadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa -UNCEF kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Rungwe.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa