Noah kibona, Rungwe Dc
Watanzania wametakiwa kuwajali watu wenye mahitaji maalumu kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kuleta ustawivu bora kwa jamii.
Rai hiyo imetolewa na Katibu tawala Wilaya ya Rungwe bwana Nkondo Bendera wakati wa maadhimisho sikukuu ya walemavu duniani ambayo kiwilaya ilifanyoika katika viwanja vya halmashauri ya wilaya ya Rungwe.
Akifafanua zaidi bwana Bendera aliongeza kuwa asilimia 20 ya watu masikini duniani ni walemavu hivyo juhudi za pekee zinatakiwa kuongezwa kwa watu wenye ulemavu ili kuboresha maisha yao ikiwa ni pamoja na kupewa mikopo isiyo na riba na mazingira wezeshi ya kupata elimu na stadi za maisha.
Hata hivyo imeelezwa kuwa asilimia 2 ya mapato na ndani ya Halmashauri yamekuwa yakielekezwa kwenye kundi maalumu la watu wenye ulemavu ambapo hukopeshwa bila riba kwenye vikundi na mtu mmoja mmoja.
Akitoa ufafanuzi zaidi mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Rungwe DR. Lawrence Kibona amesema kuwa fedha hizo zimekuwa zikiingizwa kwenye mfuko wa walemavu kwa lengo la kuchochea maendeleo kwa watu wenye mahitaji maalumu. “Kwa misimu yote halmashauri imekuwa ikiingiza fedha hizo kwa wakati kwa lengo la kuchochea maendeleo katika kundi hilo maalumu” aliongeza.
Aidha mwenyekiti wa shirikisho la watu wenye ulemavu wilaya ya Rungwe Bwana Emu Kasote amesema kuwa kuto rudisha mikopo kwa baadhi ya vikundi kumechangia kukwama kwa mkakati mahususi wa kuhakikisha makundi yote yananufaika na mfuko wa walemavu.
Pamoja na hayo bwana Kasote ameomba kuandaliwa miundo mbinu wezeshi ya walemavu ikiwemo vivuko vya walemavu , vizimba vya biashara, na usafiri ili kuwasaidia kufanikisha malengo waliyojiwekea ikiwemo na kupewa watalamu wa lugha ya alama kwa vizwi hasa katika maeneo maalumu kama hospitali, na mahakamani .
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa