Wakuu wa shule za sekondari wakiwa katika kikao ambacho kimefanyika katika ukumbi wa kituo cha walimu wa sekondari kilichopo Tukuyu mjini. Lengo la kikao hicho ni kuangalia changamoto walizokuwa nazo kabla ya kufunga shule kwa muhula wa kwanza wa masomo na kuweka mikakati mipya kwa muhula wa pili wamasomo ambao umeanza Leo tarehe 2/7/2018. Jumla ya walimu wakuu 36 walihudhuria kikao hicho. Kikao hicho kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali ambao ni wadau wa elimu wilayani.
Afisa maendeleo ya jamii bibi Rachael Mbelwa amewakumbusha wakuu wa shule wajibu wao wakufanya kazi kwa weredi pia kuzingatia nidhamu kwa walimu mashuleni na wanafunzi.
Mkaguzi wa hesabu za ndani ndugu Msigwa amesisitiza wakuu wa shule kuweka taarifa sahii za fedha zitumiwazo mashueni na kuzingatia matumizi sahihi ya fedha hizo katika shughuli ilizopangwa .
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa