WAKULIMA RUNGWE KUNUFAIKA NA KITUO JUMUISHI CHA MAZAO YA BUSTANI.
Kesho tarehe 24.7.2024 Mkandarasi anatarajiwa kukabidhiwa rasmi eneo la Mradi wa ujenzi wa kituo jumuishi cha kuongeza thamani mazao ya Bustani kilichopo Kijiji cha Nkunga kata ya Nkunga Barabara ya Karasha-Ibililo takribani Km 1 kutoka Soko la ndizi Karasha.
Kituo kitakuwa na uwezo wa kukusanya kuchambua,kupanga madaraja na kuhifadhi mazao kama parachichi na hatimaye kusafirishwa kwenda katika masoko ya ndani na nje ya nchi.
Ujenzi unatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi Billion 2.9 mpaka kukamilika kwake.
Kituo hiki mara kitapokamilika kitapunguza upotevu wa mazao ya bustani, kuimarisha ubora na hivyo kutoa fursa ya ushindani katika soko la kimataifa.
Hii ni fursa kwa wakulima wa matunda hasa parachichi kwani hatua hii pia itaboresha bei ya zao hili la kimkakati wilayani Rungwe na wafanyabiashara kuwa na eneo maalumu la ukusanyaji na upakiaji wa parachichi kwa ufanisi mkubwa.
********************"
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa