Wakazi wa wilaya ya Rungwe wamekumbushwa kuendelea kupata chanjo dhidi ya COVID 19 (CORONA) ikiwa ni hatua sahihi ya kupata kinga na hivyo kujipa nafasi bora ya kuwa na afya nzuri na hivyo kushiriki katika shughuli za maendeleo ya kila siku
.Rai hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mhe. Dkt Vicent Anney wakati akiongea na wananchi wa kata ya Ikuti katika maeneo tofauti.Aidha ameagiza wakazi wa wilaya ya Rungwe kuachana na imani potofu dhidi ya chanjo hiyo na kuwa kuendelea kuwasikiliza wapotoshaji itahatarisha maisha yao huku serikali imewapatia chanjo bila gharama yeyote.
Chanjo hiyo inapatikana katika Hositali ya wilaya Tukuyu, kituo cha afya Masukulu, Ikuti, Zahanati ya Ndaga na hospitali ya Igogwe.
Katika ziara hiyo mamia ya wakazi wa kijiji cha Lyenje, Ikuti na Kyobo wamejitokeza kupata chanjo hii
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa