Kamati ya lishe imeketi Leo tarehe 1.2.2023 huku ikibainishwa kuwa jumla ya Wanawake 15,221 wenye watoto wa umri wa miezi 0-23 wameelimishwa dhidi ya lishe bora kwa kipindi Cha Mwezi January 2023 sawa na asilimia 76%
Aidha jumla ya watoto 14,124 wameweza kufikiwa kwa ajili ya ufuatiliaji wa Maendeleo ya ukuaji wa Mtoto.
Pamoja na mafanikio makubwa yaliyofikiwa imeelezwa kuwa baadhi ya wazazi na walezi wanaendelea kuwaanzishia chakula mapema watoto kabla ya kufikisha umri wa miezi sita naa hivyo kusababisha watoto kukumbwa na utapiamlo.
Hali hii husabanishwa na watoto kuharisha mfululizo ikisababishwa utumbo kutokuwa tayari kumeng'enya chakula
Hata hivyo elimu imeendelea kutolewa ili kuepukana na kadhia hiyo.
Katika hatua nyingine imeelezwa kuwa kumekuwa na ongezeko la wanafunzi wanaokula chakula Cha mchana shuleni ambapo ulaji umepanda mpaka kufikia asilimia 100% kwa madarasa ya mitihani lengo likiwa ni kuwafikia wanafunzi wote.
Mathalani shule ya Msingi Bagamoyo, Bujinga,Nuru, Bujela, Njikula, Nsongola, Segela, Bulyaga, Madaraka, Ibigi, Katumba, lyenje, Kyobo, Ikuti, Mpandapanda na nyingine nyingi wanafunzi wake wanaokula kwa asilimia 100%
Hata hivyo shule, taasisi pamoja na kaya zote zimehamasishwa kuendelea kulima bustani,matunda, uhakika wa chakula chenye viini lishe hii ni pamoja na ufugaji wa samaki ili kuongeza na kuboresha lishe ya jamii.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa