Kilimo cha viazi mviringo kimeendelea kuwanufaisha wakazi kijiji cha Ntokela kata ya Ndanto Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe.
Uzingatiaji wa kanuni za kilimo bora, na soko la uhakika la viazi limempa nafasi kijana, Ezra Mapembelo kujenga nyumba ya kisasa kwa muda mfupi.
Ezra anatoa wito kwa vijana wenzake katika wilaya ya Rungwe kufanya kazi kwa bidii, kupanga matumizi sahihi ya kipato chao, kuwa na uelewa mpana wa maisha ya kila siku, Kujitambua, na kushirikiana na jamii katika shughuli za maendeleo kijijini na serikali kwa ujumla.
Ezra anataja kuwa nyumba yake ametumia zaidi ya shilingi Million 37, fedha iliyosaidia kujenga nyumba hiyo yenye vyumba viwili vya kulala, sebule na jiko.
Kijiji cha Ntokela ni moja ya vijiji vinavyokua kwa kasi zaidi wilayani Rungwe. Vijiji vingine ni Nzunda, Ndaga na Goye ambapo kijiji cha Nzunda kimebuni na kujenga soko la kisasa linalotarajia kutumia zaidi ya shilingi million 100.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa