KATA YA KINYALA YANUFAIKA NA KITUO CHA AFYAUhamasishaji wa ujenzi wa kituo cha afya kata ya Kinyala umefanyika leo asubuhi tarehe 24.09.2021 katika kijiji cha Lubigi katika kata hiyo.
Kituo hicho kinachotarajia kugharimu shilingi million 201,573,374/= ( Mapato ya ndani) kitavinufaisha vijiji 6 vyenye jumla ya wakazi 16,964 katika kata hiyo na maeneo ya jirani hususani Wilaya ya Mbeya vijijini.
Akihamasisha ushiriki wa wananchi katika ujenzi wa kituo hicho, Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Dk Vicent Anney ameagiza kila mkazi wa kata hiyo kushiriki kikamilifu ikiwa ni pamoja na kuchangia nguvu kazi ili kupunguza gharama ya ujenzi na hivyo fedha ya ziada kutumika katika ukamilishaji wa miundo mbinu mingine.
Aidha ameonya wananchi kutojihusisha na uwizi wa vifaa vya ujenzi wa kituo hicho na kuwa kwa kufanya hivyo itakwamisha mradi na hatimaye kushindwa kukamilika kwa wakati.
Dkt Vicent ameendelea kuwakumbusha wakazi wa kata hiyo kupata chanjo dhidi ya COVID 19 ili kujihakikishia kinga dhidi ya CORONA pamoja na na wananchi kushiriki zoezi la sensa ambalo linatarajiwa kufanyika hivi karibuni kwa kutoa taarifa sahihi ili kuipa nafasi serikali kupanga shughuli za maendeleo ikiwa ni pamoja na utoaji huduma stahiki kwa wananchi wake.
Katika hamasa hiyo Mbunge wa Jimbo la Rungwe Mhe. Antony Mwantona ameahidi kutoa ushirikiano mkubwa kuhakikisha kituo hicho kinakamilika kwa wakati.Amesema kwa sasa (Leo) anatoa mifuko ya saruji 50 kwa kila shule ya msingi kisoko na kisumba na mabati 100 kwa shule ya sekondari Kinyala ikiwa ni sehemu yake ya ahadi aliyoitoa awali.
Baada ya hapo nguvu atazihamishia katika kituo hicho cha afya ikiwa hatua ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Katika hatua ya awali kituo hicho cha afya kitakuwa na majengo ya wagonjwa wa nje (OPD), Jengo la Wazazi (maternity) , vyoo na kichomea taka.
Majengo mengine yataendelea kukalishwa kulingana na upatikanaji wa fedha
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa