Kupitia Radio Chai 105.7 Mhz, Wafanyabiashara katika Halmashauri ya wilaya ya Rungwe wamekumbushwa kuendelea kuhuisha Leseni zao za biashara ikiwa ni pamoja na kupata leseni mpya kwa wale ambao wameshindwa kufanya hivyo ili kujijengea mazingira mazuri ya kufanya shughuli zao za kila siku katika hali ya utulivu.
Kuelekea Mwisho wa mwaka wa fedha Kiserikali, afisa biashara wilaya bwana Lodrick Yesaya Mwakisole pia ameomba wapangaji wanaotumia vibanda vya halmashauri kuhakikisha wanalipa kodi yao mapema ikiwa ni pamoja na na wale wanaotakiwa kulipa ushuru wa huduma (service levy) kufanya hivyo ifikapo june 23 mwaka huu.
Pamoja na hayo bwana Mwakisole amesema kuwa wajasiriamali wote katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe wenye nia ya kushiriki maonesho ya sabasaba mwaka huu ambayo kitaifa yatanyika jijini Dar es salaam wanatakiwa kufika katika ofisi ya Mkurugenzi Kitengo cha Biashara ili kupata namna bora ya kushiriki maonesho hayo .
Aidha amewakumbusha kuendelea kupata vitambulisho vya ujasiriamali ambavyo kwa sasa vinapatikana kwa njia ya mfumo ambapo kupitia simu ya mkononi mnufaika anaweza kujisajili mwenyewe. Pia anaweza kupata msaada wa karibu kupitia kwa watendaji wa kata waliopo katika maeneo yao. Kitambulisho hiki tofauti na cha awali kina picha ya mnufaika.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa