Msimu wa uvunaji wa mahindi unaendelea katika maeneo takribani yote katika halmashauri ya wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.
Wakulima wanashauriwa kuvuna kwa wakati , Kuyakausha kwa joto la kutosha na kuyatunza vizuri ili kuepukana na SUMU KUVU hali inayotokana na kuyaacha mahindi katika hali ya unyevunyevu na hivyo kusababisha kuoza na kupata fangasi.
Athari ya Sumu kuvu (fangasi) ni kusababisha walaji kupata kansa na hivyo kupelekea vifo ambavyo vingiweza kuzuilika kwa kufuata taratibu sahihi za uvunaji na uhifadhi wa mahindi.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa