Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Mhe. Dkt Vicent Anney Leo tarehe 13.01.2023 ameongoza zoezi la ugawaji wa vishikwambi (Tablets) kwa walimu wa shule za Msingi na Sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ikiwa ni nyezo muhimu ya kuboresha Ufundishaji na ujifunzaji kwa Wanafunzi.
katika zoezi hilo Mhe. Anney ameagiza kila Mwalimu kwenda na kuvitumia vishikwambi hivyo kwa malengo mahususi yaliyotarajiwa huku akieleza kuwa kila Mwezi Kutakuwa na uhakiki wa uwepo na Matumizi sahihi ya vifaa hivyo katika shule zote.
Mhe. Anney ametaja matumizi ya vishikwambi hivyo kuwa ni pamoja na kuandaa Masomo kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya maarifa kwa njia ya mtandao, na kuandaa taarifa na kuzituma katika ngazi mbalimbali za kitaluma.
Katika hatua nyingine Mhe. Anney ameagiza wanafunzi wote WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA na kidato Cha kwanza sambamba na Wale waliofikia umri wa kusajiliwa darasa la kwanza kufanya hivyo na kupokelewa na shule husika bila masharti yeyote ikiwa ni haki ya Msingi na stahiki kwa mwanafunzi.
Akifungua kikao hicho Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Bwana Castory Makeula ametaja jumla ya vishikwambi 1131 kuwa vitapelekwa katika shule mbalimbali ili kuboresha elimu na hivi karibuni vingine vinatarajia kupokelewa kutoka Serikali kuu na vitasambazwa shuleni.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa