VIKUNDI VINAVYOJIZOLEA MAPATO YA NDANI YA HALMASHAURI.
Kupitia mikopo ya vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu, Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe imetoa mkopo usio na riba kwa Kikundi Cha Milimani Block wenye thamani ya shilingi Million 36 kwa ajili ya ununuzi wa Machine ya kufyatulia tofari.
Mkopo huu ni sehemu ya asilimia 10% ya mapato ya ndani ya Halmashauri.
Mashine hiyo yenye uwezo wa kufyatua matofari 2000 kwa siku imeongeza ajira kwa Vijana sambamba na usambazaji wa bidhaa hiyo kwa wakazi wa Wilaya ya Rungwe pamoja na miradi mbambali ya umma ya ujenzi.
Kikundi hicho kilichopo kata ya Kawetere Barabara ya Tukuyu- Kyela kipo mbioni kununua Lori litakalosaidia kusambazwa tofari kwa wateja wao kwa urahisi zaidi.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa