Jumla ya shilingi million 231,612,800/=zimekabidhiwa kwa AMCOS ya UWAMARU iliyopo kata ya Kyimo na Shirika la UNITED STATE AFRICAN DEVELOPMENT FOUNDATION (USADF) ikiwa ni ruzuku itakayoboresha muungano huo wa wakulima.AMCOS hiyo inayojishughulisha na kilimo, ununuzi na usafirishaji wa Parachichi ina jumla ya wanachama 265 ambao ni wakulima wa zao hilo.
Ruzuku hiyo itatumika kuchochea kilimo cha parachichi kwa kugharamia mafunzo kwa wakulima, ujenzi wa jengo la kuhifadhia mali mbichi (coldroom), ununuzi wa pikipiki, jenereta, uboreshaji wa miche, na ajira kwa watumishi wapya wa mradi huo.
Mkuu wa wilaya ya Rungwe Mhe. Dkt. Vicent Anney (kulia kwenye picha) ndiye alikuwa mgeni rasmi na kushuhudia utilianaji saini wa makabidhiano hayo amabapo ameonya wanufaika kutotumia vibaya ruzuku hiyo badala yake fedha hizo ziboreshe zao la parachichi, uanzishwaji wa viwanda vya usindikaji sambamba na kushirikiana na Makampuni makubwa kama KUZA AFRIKA ili kujengeana uwezo na kupanua fursa ya masoko nje ya nchi.
Meneja mradi wa USADF nchini Tanzania bwana Gilliad Nkini ameomba wanufaika wa ruzuku hiyo kuzingatia taratibu za manunuzi ikiwa ni pamoja na mafunzo mbinu itakayoongeza maarifa yatakayodumu hata baada ya mradi kumaliziza muda wake ( mwaka mmoja)
Hata hivyo Mwenyekiti wa AMCOS hiyo Bwana Kayusi Msigwa ametaja sifa zilizosababisha kupata ruzuku hiyo kuwa ni pamoja na:
1. Kupata hati safi ya ukaguzi
2.Uwepo wa ekari mbili za ardhi mali ya chama
.3 Usimamizi mzuri wa mashamba ya wakulima.
4. Kuwaunganisha wakulima na kuzalisha kwa tija.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa