Noah kibona, Rungwe Dc
Imeelezwa kuwa uuzaji wa barakoa usiofuata kanuni za afya unaweza kuchangia maambukizi na kuenea kwa virusi vya COVID 19 miongoni mwa watumiaji nchini Tanzania.
Rai hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji halmashauri ya wilaya ya Rungwe bibi Loema Peter wakati akiongea na watumishi wa halmashauri hiyo ikiwa ni sehemu ya kupeaana elimu dhidi ya ugonjwa hatari wa corona ambao kwa sasa umefanikiwa kuenea ulimwenguni kote.
Aidha bibi Loema amewaomba wauzaji wa barakoa kutoruhusu wateja wao kujaribisha na kisha kuirudisha kama haimtoshi kwani kwa kufanya hivyo itachangia maambukizi ya COVID 19.
Pamoja na hayo amesisisitiza kuwa uvaaji wa barakoa kwa kuiegesha chini ya kidevu na juu ya paji la uso na kisha kuirudisha mdomoni inaweza kuwa moja ya ukiukwaji wa kanuni za uvaaji wa barakoa miongoni mwa watumiaji.
Akichangia zaidi Mganga mkuu wa halmashauri ya wilaya ya Rungwe Dr. John Mrina amewaomba watumiaji kuhakikisha wanavaa barakoa hizo siyo zaidi ya masaa manne na kisha kuziteketeza ili kuepuka uwezekano wa kuenea kwa virusi hivyo.
Hata hivyo Dr..Mrina amewaasa wakazi wa wilaya ya Rungwe kuhakikisha wanakula vyakula vyenye viini lishe kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kuimarisha kinga ya mwili.
Katika halmashauri ya wilaya Rungwe zoezi la upimaji wa joto kubaini dalili za ugonjwa wa Corona unaendelea maeneo mengi ikiwemo hospitali ya wilaya Tukuyu, ambapo kituo cha afya Isongole kimeteuliwa kutumika kuwahudumia washukiwa wa Covid 19.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa