• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
Rungwe District Council
Rungwe District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa naSerikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utumishi na Utawala
      • Mipango, Uchumi na Takwimu
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, U mwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Maendeleo na Ustawi wa Jamii
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maji
      • Ujenzi na Zimamoto
      • Usafishaji na Mazingira
      • Ardhi na Maliasili
    • Vitengo
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Sheria
      • Tehama na Mahusiano
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Utunzaji Nyuki
  • Uwekezaji
    • Uzalishaji wa Maziwa
    • Kiwanda Cha Matunda
    • Vivutio vya Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • Ardhi na Maliasili
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
    • Ratiba
      • Mikutano ya Madiwani
  • Miradi
    • Miradi iliyoidhinishwa
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu za Maombi
    • Katiba Pendekezwa
    • Mihutasari
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Maktaba ya Picha
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma
    • Matukio
    • Habari
    • Makala

UTEKELEZAJI WA ILANI WAWASILISHWA

Imewekwa Tarehe: May 30th, 2025

HALMASHAURI YA (W) RUNGWE YAWASILISHA  UTEKELEZAJI  ILANI YA UCHAGUZI 2020/25


Halmashauri ya wilaya ya Rungwe imewasilisha Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi   CCM  ( 2020-2025)  kwa Wakazi wa Wilaya ya Rungwe mbele ya Wajumbe wa chama hiki Tawala nchini.


Uwasilishaji umefanyika katika Halmashauri ya Busokelo ambapo Halmasauri ya Rungwe na Busokelo zimewasilisha kupitia Kamisaa wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Rungwe  Mhe. Jaffar Haniu.


Wilaya ya Rungwe huundwa na Halmashauri Mbili ambazo ni Rungwe na Busokelo na Makao makuu yapo katika Mji wa Tukuyu.


Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe kama zilivyo taasisi zingine imeendelea na utekelezaji wa wa Ilani huku ikisimamia ipasavyo makusanyo na matumizi ya fedha  kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi.


Kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Halmashauri imepokea kiasi cha shilingi 6,279,179,328.63 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta ya afya, elimu maendeleo ya jamii kilimo na mifugo.


Aidha Halmashauri imefanikiwa kukusanya mapato yake ya ndani kutoka asilimia 96% mwaka wa fedha 2021/22 Mpaka kufikia asilimia 103% kwa mwaka wa fedha 2023/24.


Katika sekta ya afya Ilani imetekelezwa kwa ujenzi jengo la wagonjwa wa nje, Wodi ya wanawake na wanaume na ofisi katika Hospitali ya wilaya Tukuyu kwa zaidi ya shilingi Billion 2.


Pamoja na hayo vituo vya afya Kiwira, na Masoko imeshuhudiwa vikijengwa kwa zaidi ya shilingi Billion 1


Zaaidi ya hayo imeshuhudiwa ongezeko la zahanati kutoka 37 mwaka 2020 hadi zahanati 41 mwaka 2024.Vituo vya afya 7 mwaka 2020  hadi vituo 9 disemba 2024.


Hali hii imesaidia kupungua kwa vifo vya mama na mtoto kutoka wastani wa vifo 60/100,000 hadi vifo 23/100,000 mwaka 2024 ukilinganisha na wastani wa kitaifa 454/100,000


Katika Sekta ya elimu Msingi Vyumba vya madarasa vimeongezeka kutoka 1,011 mwaka 2020 hadi vyumba 1,157 Disemba 2024


Ufaulu umeonngezeka kutoka asilimia 85.27% mwaka 2020 kwenda 96.58% mwaka 2024


Ili kusogeza huduma bora ya elimu kwa wananchi serikali imefanikiwa kuanzisha shule mpya ya Kibumbe, Umoja, Ushirika, Chief Mwanjali, Matale, Halanzi na Saswago.


Kwa upande wa Sekondari Kiwango cha ufaulu kidato cha nne kimepanda kutoka 93.57% mwaka 2020 mpaka kufikia asilimia 95.5 mwaka 2024


Kidato cha sita ufaulu umefikia asilimia 100% mwaka 2024 ili hali mwaka 2021 ufaulu ulikuwa asilimia 99.5%  tu.


Serikali imefanikiwa kuanzisha shule mpya kama Kibisi, Isaka, Msasani, Kisondela, Kawetere,  Lukata, Isuga, Kikota na Kyobo.


Kwa upande wa maendeleo ya Jamii Halmashauri imefanikiwa kupambana na na maambukizi ya  UKIMWI ngazi ya jamii kutoka 9.3% na kufikia 9.0% mwaka 2024


Halmashauri imefanikiwa kukopesha vikundi vya Vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kutoka  shilingi 848,500,000 mwaka wa  fedha 2020/2021 hadi kufikia shilingi  1,867,527,500 kwa mwaka 2023/24 (Disemba 2024)


Fedha hizi zimesaidia wananchi kujikwamua kutoka katika makucha ya umasikini kwa kuanzisha viwanda vidogovidogo, Ufugaji, kilimo, usafirishaji, na  biashara .


Halmashauri pia imefanikiwa kupanua Sekta ya Kilimo, na Mifugo hii ni kutokana na Hali ya hewa nzuri na udongo wenye rutuba.


Hali hii imesaidia sekta ya kilimo kuchangia asilimia 90% ya Uchumi wa wilaya ya Rungwe


Mazao muhimu ni pamoja na kahawa, chai, kakao, parachichi, viazi mviringo na ndizi.


Mathalani uzalishaji wa kahawa umepanda kutoka tani 647.7 mwaka 2020 hadi tani 1,226.5 mwaka 2024 sawa na ongezeko la asilimia 89.3


Jumla ya tani 6,537.8 imesambazwa kwa wakulima huku wakulima 39,650 wakisajiliwa katika mfumo wa mbolea za ruzuku.


Kutokana na kukua kwa njia bora ya ufugaji na uhimilishaji wa mifugo hasa ngo'mbe Jumla ya lita 64,800,000 zinazalishwa kwa mwaka sawa na wastani wa lita 1800,000 kwa siku na wastani wa uzalishaji wa ngombe mmoja kwa siku ni lita 10 hadi 15


Kiasi kinachouzwa kwenye soko rasmi ni lita 33,100 kwa siku ambapo kampuni ya ASAS hununua kiasi cha lita 28,000 kila siku. Kiasi kinachobaki huuzwa katika soko la kwaida.


Matangazo

  • ORODHA YA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE SEMINA NAFASI YA WAANDISHI WASAIDIZI NA BVR December 19, 2024
  • ORODHA YA MAJINA YA AKIBA NAFASI YA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI December 19, 2024
  • TANGAZO BARAZA LA MADIWANI April 27, 2021
  • TANGAZO LA AJIRA ZA MKATABA June 10, 2021
  • Onesha Vyote

Habari Mpya

  • ELIMU YA UTUNZAJI VYANZO VYA MAJI YAHAMIA KIWIRA

    May 31, 2025
  • UTEKELEZAJI WA ILANI WAWASILISHWA

    May 30, 2025
  • KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YAKAGUA MIRADI

    May 30, 2025
  • MHE.MCHENGERWA AONGOZA KIKAO CHA MAAFISA HABARI

    May 24, 2025
  • Onesha Vyote

Video

Vivutio vya Utalii
Picha Mjongeo Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Ofisi ya Mkuu wa Mkoa
  • TAMISEMI

Vinganishi Linganifu

  • OR TAMISEMI
  • Wizara ya Elimu na Ufundi
  • Sekretarieti ya Ajira Utumishi wa Umma

Kipimo cha Wateja Duniani

world map hits counter

Wateja Waliotembelea

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana Nasi

    Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB

    Sanduku la Posta: Box 148

    Simu: 025 255 2586

    Simu ya Kiganjani:

    Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Huruhusiwi
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa