Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Rungwe bibi Loema Peter amekutana na viongozi wa soko la Kiwira na kutatua kero mbalimbali za soko hilo.
Aidha bibi Loema amewaomba viongozi hao kuendelea kuwasisitizia wafanyabiashara wa soko hilo kuchukua vitambulisho vya Wajasiriamali ili kuepukana na bugugha inayoweza kujitokeza wakati watakapokuwa wanatekeleza majukumu yao ya kila siku mahali popote nchi nzima.
Hata hivyo amewaonya wafanyabiashara hao kuto changia kitambulisho kimoja zaidi ya mtu mmoja kwani kwa kufanya hivyo wanaipotezea mapato serikali na hivyo kushindwa kuwaletea huduma stahiki katika maeneo yao.
Pamoja na hayo amewaomba watoza ushuru kuendelea kutoa risti za kielekroniki kwa wafanyabiashara hao na kuacha kutoza ushuru wenye nia ya kuleta imla na hivyo kusababisha watu kuichukia serikali yao tukufu.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa