Mwaka 1891 kanisa la kwanza lilijengwa katika kijiji cha Ilolo maarufu kama Kisungu ( Rungwe Mission) eneo linalotajwa kama chimbuko la Kanisa la Moravian Tanzania.
Halmashauri ya wilaya ya Rungwe kupitia Kitengo cha Maliasili na Utalii imeendelea kutambua na kuhamasisha wadau kuwekeza katika sekta ya utalii wa utamaduni, maji, misitu, Milima na sasa kilimo.
Kanisa la Moravian sasa limejenga jengo la Makumbusho lililobeba amali na historia ya utamaduni wa kabila la Wanyakyusa na Wandali kutoka katika wilaya ya Rungwe , Kyela na Ileje.
Eneo lingine la ibada la kale zaidi ni Msikiti uliojengwa katika eneo la Kisiba kando ya Ngome ya Kijerumani na ziwa Kisiba kijiji cha Lwifwa kata ya Kisiba.
Msikiti huu unatajwa Kuwa ndiyo wa kale zaidi mkoani Mbeya na ulijengwa na wapagazi waliotumika kubeba mizigo ya wazungu wakitokea lango kuu la Bagamoyo mkoani Pwani.
Msikiti huu bado upo na unaendelea kutoa huduma ya kiroho.
Tembelea Rungwe District Council ujionee vivutio lukuki
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa