Magonjwa yasiyopewa kipaumbele Tanzania yamewakutanisha Makatibu tawala, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi na watafiti katika Halmashauri nne lengo likiwa ni kujadili mafanikio yaliyofikiwa kutokomeza magonjwa haya ikiangaziwa zaidi katika ugonjwa wa USUBI.
Kikao hicho kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe kimejumuisha Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Kyela, Ileje na Busokelo.
Katika kikao hicho taasisi ya utafiti wa magonjwa ya Binadamu (NIMRI) imeeleza kuwa tangu mwaka 1980 tafiti zimekuwa zikifanyika kupitia kituo cha Tukuyu na kubaini kuwa ugonjwa wa USUBI una madhara kwa jamii.
Baadhi ya madhara ya ugonjwa wa usubi ni pamoja na kupunguza nguvu za kuona, kuwa kipofu kabisa, na kiuchumi taifa linapunguza nguvu ya uzalishaji Mali katika jamii.
Dalili za Usubi ni mgonjwa kupata muwasho mithili ya mtu aliyeumwa na Mbu (Muwasho usioisha).
Ugonjwa huu husambazwa na nzi mweusi ambaye hutaga mayai na kuzaliana katika maji/mito inayotembea kwa kasi.
Baada ya kuzaliana nzi huruka mpaka kufikia km 15 kuelekea makazi ya watu na hivyo wakazi waliopo kando ya mito wapo hatarini kuambukizwa.
Utafiti umeonesha kuwa mito iliyoathirika zaidi ni pamoja na Lufiliyo, Mbaka, Kiwira, Songwe na Lumbira ulipo Ludewa Mkoani Njombe.
Maeneo yaliathirika zaidi ni ukanda wa chini ambapo una joto la wastani au zaidi.
Kupitia kituo cha Tukuyu Mpango wa kutokomeza ugonjwa huu ulianza kufanyiwa kazi ambapo mwaka 2000-2005 dawa aina ya IVERMECTIN ilianza kusambazwa katika jamii kwa njia ya kumeza pamoja na kunyunyiza katika mito na mpaka Sasa maambukizi yamepungua mpaka kufikia asilimia 80%•
Nchini Tanzania maeneo mengine yaliyoathirika na USUBI ni pamoja na Mkoa wa Morogoro, Tanga na Ruvuma.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa