Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe Bwana Renatus Mchau ameongoza jopo la Watalamu katika ukaguzi wa miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule nne za Sekondari shule ya Msingi Moja pamoja na zahanati mapema Leo tarehe 21.11.2022.
Shule hizo ni pamoja na Sekondari ya Kyobo, Nkunga, Isaka na Ndembela one na shule ya Msingi Ikuti.
Zahanati iliyokaguliwa ni Kakindu iliyopo katika Kijiji Cha Lupepo kata ya Lupepo.
Ikumbukwe kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imetoa kiasi Cha shilingi million 200 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa.
Shule zilizonufaika ni pamoja na Isaka, Kayuki, Igogwe, Kibisi, Ndembela one, Nkunga, Kyobo na Ziwa Ngosi.
Katika shule zote ujenzi upo katika hatua ya ukamilishaji hali itakayosaidia wanafunzi watakaojiunga na kidato Cha kwanza Mwakani January 2023 kupata mazingira mazuri ya kusomea na kujifunza.
Akikagua miradi hiyo Bwana Mchau ameagiza kamati zinazosimamia ujenzi huo kufanya kazi usiku na mchana ili kusaidia miradi hiyo kukamilika kwa wakati na hivyo kuleta tija na maendeleo kwa wanafunzi.
Aidha amearifu kuwa tayari zahanati ya Kakindu imepata kiasi Cha shilingi million 25 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba hali itakayosaidia upatikanaji wa huduma ya matibabu katika mazingira ya karibu zaidi.
Hata hivyo wakazi wa Kitongoji Cha Kakindu wamepongeza juhudi za Serikali katika kuhakikisha wanapata afya bora na stahiki kwa kuwapatia kiasi Cha shilingi million 50 kwa ajili ya ukamilishaji wa zahanati hiyo sambamba na million 50 zingine wanazotarajia kuzipata hivi karibuni kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya watumishi.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa