Ujenzi wa vyumba 55 vya madarasa katika shule 18 za sekondari umefikia katika hatua nzuri ambapo madarasa yote yanatarajiwa kukabidhiwa kwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Rungwe baada ya mafundi waliokabidhiwa ujenzi huo kuyakamilisha leo .
Hii ni kufuatia agizo alilolitoa Mkurugenzi Mtendaji Bwana Renatus Mchau mapema wiki iliyopita kuwa miradi yote iwe imekamilika ifikapo tarehe 27.12.2021 ili kuwapa nafasi wanafunzi wa kidato cha kwanza kuanza masomo yao mapema mwakani januari 2022.
Huu ni utekelezaji wa Mpango wa Ustawi wa Taifa na Mapambano ya UVIKO 19
Ujenzi wa vyumba hivyo utajumuisha viti na meza 50 kwa kila chumba hii ikiwa ni pamoja na meza na kiti cha Mwalimu.
Ujenzi huu unatarajia kugharimu kiasi cha shilingi Billion 1.1 fedha iliyotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa