Kamati ya Fedha Uchumi na Mipango imeendelea na ukaguzi wa miradi ya Maendeleo Leo tarehe 22.12.2022 kwa kukagua miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule za sekondari.
Shule zilizokaguliwa ni pamoja na shule mpya ya Kibisi na Igogwe sambamba na shule ya Ndembela one na Kayuki.
Jumla ya vyumba vitano vimekaguliwa Leo vyenye thamani ya shilingi million 100 pamoja na viti/ meza 250.
Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe ilipokea kiasi Cha shilingi million 200 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 10 vya madarasa kwa shule 8 za Sekondari pamoja na utengenezaji wa meza na viti 500.
Kamati imejiridhisha na hatua ya ujenzi iliyofikiwa na kupongeza namna kamati za ujenzi,manunuzi, na mapokezi zilivyofanya kazi kwa weledi ikiwa ni hatua muhimu kuhakikisha wanafunzi wote WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA na kidato Cha kwanza wanapata sehemu nzuri ya kusomea na kujifunzia.
Awali Amina Mwaihojo mkazi wa Kijiji Cha katabe kata ya Kyimo ameishukuru Serikali kuwajengea shule mpya ya Kibisi hatua itakayowapunguzia watoto wao kufuata huduma ya elimu katika shule ya Sekondari Kyimo na Lupoto.
" Mtoto wa kaka yangu anatembea kwa miguu kutoka Kalalo mpaka Sogea(Kyimo) zaidi ya kilometa 5 lakini saivi aaaaah! anaenda hapo juu tu" Ameeleza.
Rungwe inatarajia kufungua shule mpya nne za Sekondari ambazo ni Kibisi , Msasani , Igogwe na Isaka.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa