Zaidi ya shilingi million 500 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa kituo cha afya katika kata ya Kyimo zikiwa ni fedha zilizotolewa na serikali ya Jamhuri ya mungano wa Tanzania.
Kituo hicho kilichopo mtaa wa Ikata kijiji cha Kyimo (K.K) utajumuisha jengo la wagonjwa wa nje (OPD), Jengo la wagonjwa wa Ndani(IPD), Jengo la wazazi na upasuaji, Jengo la kufulia, Kichomea taka, Choo, mfumo wa taka pamoja na njia ya kuunganisha majengo.
Ujenzi wa kituo hiki utakuwa ni ufumbuzi wa tatizo la muda mrefu la upatikanaji wa huduma ya afya kwa vijiji vinavyounda kata hii ambavyo ni pamoja na Kyimo, Katabe, Syukula, Ilenge na Kibisi. na kuhudumia wakazi wanaokadiriwa kufikia 18,676 na maeneo ya jirani.
Utekelezaji wa ujenzi ulianza tarehe 26.6.2021 katika eneo la ekari 5.2 na unatarajiwa kumalizika mwezi januari 2021 na tayari kiasi cha shilingi million 78,179,650.00 Kimetumika hatua za awali za ununuzi wa vifaa, kufyatua tofali, ujenzi wa jamvi na kuinua kuta majengo manne pamoja na malipo kwa mafundi.
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa