Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Rungwe aongea na kamati ya ujenzi Kata ya Masoko
Mkurugenzi Mtendaji Bi.Loema I.Peter akiwa ameongozana na wataalamu wake toka idara za Mipango,Elimu sekondari na ujenzi walitembelea ujenzi wa bweni hilo ambao unaendelea katika kata hiyo tarehe 15/10/2018.
Mkurugenzi na wataalamu wake waliungana na kamati ya ujenzi ya Kata ikiongozwa na Mtendaji wa Kata ya Masoko, walianza kwa kugagua maendeleo ya ujenzi huo wa bweni ambalo litakuwa na uwezo wa kulaza wanafunzi 48 baada ya kukamilika, Pia walitembelea ujenzi wa vyoo matundu 4,bafu 4 ,sehemu maalumu kwa mahitaji ya watoto wa kike na sehemu ya kufulia ambapo vipo sambamba na bweni hilo.
Bweni hilo linajengwa kwa ufadhili wa Balozi wa Japan wakishirikiana na wananchi wa kata hiyo ya Masoko, ujenzi huo ulianza 22/06/2018 na utakamilika 19/06/2018.
Mkurugenzi Mtendaji alimpongeza Mkandarasi wa ujenzi huo kampuni ya SITOSA kwa mwenendo mzuri wa ujenzi huo. Aidha alimtaka aongeze kasi zaidi ya ujenzi huo ili samani zinazo andaliwa ziweze kuwekwa ndani ya mabweni hayo baada ya kukamilisha ujenzi huo.
Mkurugenzi Mtendaji aliwataka kamati ya ujenzi ya Kata kutoa taarifa ya ujenzi huo ndipo iliposhindwa kutoa taarifa sahihi hasa katika suala la ujenzi wa ukuta au uzio wa bweni hilo ambapo hata kasi ya ukusanyaji mawe kwa ajili ya ujenzi huo hairidhishi ,pia kamati imeamua kubadliisha shughuli ya ujenzi wa uzio na kutaka kujenga nyumba ya msimamizi (matron) ambapo haikua imepangwa toka awali ya ujenzi huo.
Aidha Mtendaji wa Kata alisema kwamba tayari walikaa kikao kwa ajili ya mapendekezo ya ujenzi huo wa nyumba na sasa wana andaa muhtasari ili kuupeleka kwa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Rungwe.
Mkurugenzi Mtendaji aliwataka kamati hiyo ya ujenzi wafuatilie kwa makini ujenzi huo sababu ni ukombozi wa watoto wa kike katika Kata hiyo na Kata za jirani. Hivyo aliwataka kuonyesha juhudi za dhati na ushirikiano katika suala hilo na kufanya uzembe usio weza kuvumilika ambao utasababisha kuwajibishana.Pia aliishauri kamati hiyo kufanya tathmini ya kina ya gharama za ujenzi wa nyumba au uzio na kulinganishanisha na bajeti waliyonayo.
Aidha Mwenyekiti wa Kijiji aliomba msamaha kwa mapungufu yote na kuahidi kurekebisha na kuyafanyia kazi.
Aidha Afisa Mipango wa Halmashauri Bi.Husna Toni alimshauri Mkuu wa Shule arekebishe na kuandaa vizuri mazingira yanayozunguka eneo hilo la bweni ikiwa ni pamoja na upandaji wa maua.
Afisa Elimu Sekondari (W) Mwl.Musa Ally aliwataka kamati hiyo waendelee na hamasa kwa wananchi ilikukamilisha ujenzi huo wa bweni ambao ndiyo itakuwa mkombozi kwa wanafunzi wakike wa shule hiyo. Pia alita taarifa kwa kamati hiyo kuwa mfadhli wa ujenzi huo balozi wa japan atatembelea mradi huo tarehe 18/10/2018.
Baadhi ya picha za ujenzi huo;
Tukuyu Mjini-Mkabala na Benki ya NMB
Sanduku la Posta: Box 148
Simu: 025 255 2586
Simu ya Kiganjani:
Barua Pepe: ded@rungwedc.go.tz
Haki Miliki ©2021 GWF. Haki Zimehifadhiwa